1 Wakorintho Mlango 11 1st Corinthians

1 Wakorintho 11:1 1stCorinthians 11:1

Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.

1 Wakorintho 11:2 1stCorinthians 11:2

Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.

1 Wakorintho 11:3 1stCorinthians 11:3

Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.

1 Wakorintho 11:4 1stCorinthians 11:4

Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.

1 Wakorintho 11:5 1stCorinthians 11:5

Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.

1 Wakorintho 11:6 1stCorinthians 11:6

Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.

1 Wakorintho 11:7 1stCorinthians 11:7

Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.

1 Wakorintho 11:8 1stCorinthians 11:8

Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.

1 Wakorintho 11:9 1stCorinthians 11:9

Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.

1 Wakorintho 11:10 1stCorinthians 11:10

Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.

1 Wakorintho 11:11 1stCorinthians 11:11

Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana.

1 Wakorintho 11:12 1stCorinthians 11:12

Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume, vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu.

1 Wakorintho 11:13 1stCorinthians 11:13

Je! Inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa?

1 Wakorintho 11:14 1stCorinthians 11:14

Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?

1 Wakorintho 11:15 1stCorinthians 11:15

Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi.

1 Wakorintho 11:16 1stCorinthians 11:16

Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.

1 Wakorintho 11:17 1stCorinthians 11:17

Lakini katika kuagiza haya, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa hasara.

1 Wakorintho 11:18 1stCorinthians 11:18

Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki;

1 Wakorintho 11:19 1stCorinthians 11:19

kwa maana lazima kuwapo na uzushi kwenu, ili waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu.

1 Wakorintho 11:20 1stCorinthians 11:20

Basi mkutanikapo pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana;

1 Wakorintho 11:21 1stCorinthians 11:21

kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa.

1 Wakorintho 11:22 1stCorinthians 11:22

Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.

1 Wakorintho 11:23 1stCorinthians 11:23

Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,

1 Wakorintho 11:24 1stCorinthians 11:24

naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

1 Wakorintho 11:25 1stCorinthians 11:25

Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.

1 Wakorintho 11:26 1stCorinthians 11:26

Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

1 Wakorintho 11:27 1stCorinthians 11:27

Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.

1 Wakorintho 11:28 1stCorinthians 11:28

Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.

1 Wakorintho 11:29 1stCorinthians 11:29

Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili.

1 Wakorintho 11:30 1stCorinthians 11:30

Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala.

1 Wakorintho 11:31 1stCorinthians 11:31

Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa.

1 Wakorintho 11:32 1stCorinthians 11:32

Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia.

1 Wakorintho 11:33 1stCorinthians 11:33

Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo mpate kula, mngojaneni;

1 Wakorintho 11:34 1stCorinthians 11:34

mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake; msipate kukutanika kwa hukumu. Na hayo yaliyosalia nijapo nitayatengeneza.