1 Wakorintho Mlango 9 1st Corinthians

1 Wakorintho 9:1 1stCorinthians 9:1

Je! Mimi si huru? Mimi si mtume? Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Ninyi si kazi yangu katika Bwana?

1 Wakorintho 9:2 1stCorinthians 9:2

Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi muhuri ya utume wangu katika Bwana.

1 Wakorintho 9:3 1stCorinthians 9:3

Hilo ndilo jawabu langu kwa wale wanaoniuliza.

1 Wakorintho 9:4 1stCorinthians 9:4

Je! Hatuna uwezo wa kula na kunywa?

1 Wakorintho 9:5 1stCorinthians 9:5

Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?

1 Wakorintho 9:6 1stCorinthians 9:6

Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo wa kutokufanya kazi?

1 Wakorintho 9:7 1stCorinthians 9:7

Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?

1 Wakorintho 9:8 1stCorinthians 9:8

Je! Ninanena hayo kwa kibinadamu? Au torati nayo haisemi yayo hayo?

1 Wakorintho 9:9 1stCorinthians 9:9

Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Je! Hapo Mungu aangalia mambo ya ng'ombe?

1 Wakorintho 9:10 1stCorinthians 9:10

Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake.

1 Wakorintho 9:11 1stCorinthians 9:11

Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?

1 Wakorintho 9:12 1stCorinthians 9:12

Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo.

1 Wakorintho 9:13 1stCorinthians 9:13

Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?

1 Wakorintho 9:14 1stCorinthians 9:14

Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.

1 Wakorintho 9:15 1stCorinthians 9:15

Lakini mimi sikutumia mambo hayo hata moja. Wala siyaandiki hayo ili iwe hivyo kwangu mimi; maana ni heri nife kuliko mtu awaye yote abatilishe huku kujisifu kwangu.

1 Wakorintho 9:16 1stCorinthians 9:16

Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!

1 Wakorintho 9:17 1stCorinthians 9:17

Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili.

1 Wakorintho 9:18 1stCorinthians 9:18

Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.

1 Wakorintho 9:19 1stCorinthians 9:19

Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.

1 Wakorintho 9:20 1stCorinthians 9:20

Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria.

1 Wakorintho 9:21 1stCorinthians 9:21

Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.

1 Wakorintho 9:22 1stCorinthians 9:22

Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.

1 Wakorintho 9:23 1stCorinthians 9:23

Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine.

1 Wakorintho 9:24 1stCorinthians 9:24

Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.

1 Wakorintho 9:25 1stCorinthians 9:25

Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.

1 Wakorintho 9:26 1stCorinthians 9:26

Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;

1 Wakorintho 9:27 1stCorinthians 9:27

bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.