1 Wakorintho Mlango 4 1st Corinthians

1 Wakorintho 4:1 1stCorinthians 4:1

Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.

1 Wakorintho 4:2 1stCorinthians 4:2

Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.

1 Wakorintho 4:3 1stCorinthians 4:3

Lakini, kwangu mimi, si kitu kabisa nihukumiwe na ninyi, wala kwa hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hata nafsi yangu.

1 Wakorintho 4:4 1stCorinthians 4:4

Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana.

1 Wakorintho 4:5 1stCorinthians 4:5

Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.

1 Wakorintho 4:6 1stCorinthians 4:6

Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.

1 Wakorintho 4:7 1stCorinthians 4:7

Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea?

1 Wakorintho 4:8 1stCorinthians 4:8

Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi!

1 Wakorintho 4:9 1stCorinthians 4:9

Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho, kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu.

1 Wakorintho 4:10 1stCorinthians 4:10

Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye akili katika Kristo; sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.

1 Wakorintho 4:11 1stCorinthians 4:11

Hata saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa ngumi, tena hatuna makao;

1 Wakorintho 4:12 1stCorinthians 4:12

kisha twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili;

1 Wakorintho 4:13 1stCorinthians 4:13

tukisingiziwa twasihi; tumefanywa kama takataka za dunia, na tama ya vitu vyote hata sasa.

1 Wakorintho 4:14 1stCorinthians 4:14

Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya kama watoto niwapendao.

1 Wakorintho 4:15 1stCorinthians 4:15

Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.

1 Wakorintho 4:16 1stCorinthians 4:16

Basi, nawasihi mnifuate mimi.

1 Wakorintho 4:17 1stCorinthians 4:17

Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.

1 Wakorintho 4:18 1stCorinthians 4:18

Basi wengine wamejivuna kana kwamba siji kwenu.

1 Wakorintho 4:19 1stCorinthians 4:19

Lakini nitakuja kwenu upesi, nikijaliwa, nami nitafahamu, si neno lao tu waliojivuna, bali nguvu zao.

1 Wakorintho 4:20 1stCorinthians 4:20

Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.

1 Wakorintho 4:21 1stCorinthians 4:21

Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole?