1 Wakorintho Mlango 5 1st Corinthians

1 Wakorintho 5:1 1stCorinthians 5:1

Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.

1 Wakorintho 5:2 1stCorinthians 5:2

Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.

1 Wakorintho 5:3 1stCorinthians 5:3

Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.

1 Wakorintho 5:4 1stCorinthians 5:4

Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu;

1 Wakorintho 5:5 1stCorinthians 5:5

kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.

1 Wakorintho 5:6 1stCorinthians 5:6

Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima?

1 Wakorintho 5:7 1stCorinthians 5:7

Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;

1 Wakorintho 5:8 1stCorinthians 5:8

basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.

1 Wakorintho 5:9 1stCorinthians 5:9

Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi.

1 Wakorintho 5:10 1stCorinthians 5:10

Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.

1 Wakorintho 5:11 1stCorinthians 5:11

Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.

1 Wakorintho 5:12 1stCorinthians 5:12

Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani?

1 Wakorintho 5:13 1stCorinthians 5:13

Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.