1 Wakorintho Mlango 2 1st Corinthians

1 Wakorintho 2:1 1stCorinthians 2:1

Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.

1 Wakorintho 2:2 1stCorinthians 2:2

Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa.

1 Wakorintho 2:3 1stCorinthians 2:3

Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi.

1 Wakorintho 2:4 1stCorinthians 2:4

Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,

1 Wakorintho 2:5 1stCorinthians 2:5

ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.

1 Wakorintho 2:6 1stCorinthians 2:6

Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;

1 Wakorintho 2:7 1stCorinthians 2:7

bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;

1 Wakorintho 2:8 1stCorinthians 2:8

ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;

1 Wakorintho 2:9 1stCorinthians 2:9

lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.

1 Wakorintho 2:10 1stCorinthians 2:10

Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

1 Wakorintho 2:11 1stCorinthians 2:11

Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.

1 Wakorintho 2:12 1stCorinthians 2:12

Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.

1 Wakorintho 2:13 1stCorinthians 2:13

Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.

1 Wakorintho 2:14 1stCorinthians 2:14

Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.

1 Wakorintho 2:15 1stCorinthians 2:15

Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.

1 Wakorintho 2:16 1stCorinthians 2:16

Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.