1 Wakorintho Mlango 14 1st Corinthians

1 Wakorintho 14:1 1stCorinthians 14:1

Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.

1 Wakorintho 14:2 1stCorinthians 14:2

Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

1 Wakorintho 14:3 1stCorinthians 14:3

Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo.

1 Wakorintho 14:4 1stCorinthians 14:4

Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa.

1 Wakorintho 14:5 1stCorinthians 14:5

Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.

1 Wakorintho 14:6 1stCorinthians 14:6

Ila sasa, ndugu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini, isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya elimu, au kwa njia ya hotuba, au kwa njia ya fundisho?

1 Wakorintho 14:7 1stCorinthians 14:7

Hata vitu visivyo na uhai vitoapo sauti, ikiwa ni filimbi, ikiwa ni kinubi, visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kwa kinubi?

1 Wakorintho 14:8 1stCorinthians 14:8

Kwa maana baragumu ikitoa sauti isiyojulikana, ni nani atakayejifanya tayari kwa vita?

1 Wakorintho 14:9 1stCorinthians 14:9

Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana mtakuwa mkinena hewani tu.

1 Wakorintho 14:10 1stCorinthians 14:10

Yamkini ziko sauti za namna nyingi duniani, wala hakuna moja isiyo na maana.

1 Wakorintho 14:11 1stCorinthians 14:11

Basi nisipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye; naye anenaye atakuwa mjinga kwangu.

1 Wakorintho 14:12 1stCorinthians 14:12

Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.

1 Wakorintho 14:13 1stCorinthians 14:13

Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri.

1 Wakorintho 14:14 1stCorinthians 14:14

Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.

1 Wakorintho 14:15 1stCorinthians 14:15

Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.

1 Wakorintho 14:16 1stCorinthians 14:16

Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika mahali pa mjinga ataitikaje, Amina, baada ya kushukuru kwako, akiwa hayajui usemayo?

1 Wakorintho 14:17 1stCorinthians 14:17

Maana ni kweli, wewe washukuru vema, bali yule mwingine hajengwi.

1 Wakorintho 14:18 1stCorinthians 14:18

Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote;

1 Wakorintho 14:19 1stCorinthians 14:19

lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha.

1 Wakorintho 14:20 1stCorinthians 14:20

Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima.

1 Wakorintho 14:21 1stCorinthians 14:21

Imeandikwa katika torati, Nitasema na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni, wala hata hivyo hawatanisikia, asema Bwana.

1 Wakorintho 14:22 1stCorinthians 14:22

Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini lakini kuhutubu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.

1 Wakorintho 14:23 1stCorinthians 14:23

Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?

1 Wakorintho 14:24 1stCorinthians 14:24

Lakini wote wakihutubu, kisha akaingia mtu asiyeamini, au mjinga, abainishwa na wote, ahukumiwa na wote;

1 Wakorintho 14:25 1stCorinthians 14:25

siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo atamwabudu Mungu, akianguka kifudifudi, na kukiri ya kuwa Mungu yu kati yenu bila shaka.

1 Wakorintho 14:26 1stCorinthians 14:26

Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.

1 Wakorintho 14:27 1stCorinthians 14:27

Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.

1 Wakorintho 14:28 1stCorinthians 14:28

Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.

1 Wakorintho 14:29 1stCorinthians 14:29

Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue.

1 Wakorintho 14:30 1stCorinthians 14:30

Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze.

1 Wakorintho 14:31 1stCorinthians 14:31

Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe.

1 Wakorintho 14:32 1stCorinthians 14:32

Na roho za manabii huwatii manabii.

1 Wakorintho 14:33 1stCorinthians 14:33

Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.

1 Wakorintho 14:34 1stCorinthians 14:34

Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.

1 Wakorintho 14:35 1stCorinthians 14:35

Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.

1 Wakorintho 14:36 1stCorinthians 14:36

Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?

1 Wakorintho 14:37 1stCorinthians 14:37

Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.

1 Wakorintho 14:38 1stCorinthians 14:38

Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.

1 Wakorintho 14:39 1stCorinthians 14:39

Kwa ajili ya hayo, ndugu, takeni sana kuhutubu, wala msizuie kunena kwa lugha.

1 Wakorintho 14:40 1stCorinthians 14:40

Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.