Kumbukumbu la Torati Mlango 23 Deuteronomy

Kumbukumbu la Torati 23:1 Deuteronomy 23:1

Aliyejeruhika konde, au aliyekatika tupu yake, asiingie mtu huyo katika mkutano wa Bwana.

Kumbukumbu la Torati 23:2 Deuteronomy 23:2

Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana.

Kumbukumbu la Torati 23:3 Deuteronomy 23:3

Mwamoni wala Mmoabi wasiingie katika mkutano wa Bwana; wala hata kizazi cha kumi mtu wao asiingie katika mkutano wa Bwana milele;

Kumbukumbu la Torati 23:4 Deuteronomy 23:4

kwa sababu hapo mlipotoka Misri hawakuwalaki na chakula wala maji njiani; na kwa kuwa walimwajiri juu yako Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyo Mesopotamia, aje akuapize.

Kumbukumbu la Torati 23:5 Deuteronomy 23:5

Lakini Bwana, Mungu wako, hakukubali kumsikiza huyo Balaamu; Bwana, Mungu wako, aliyageuza yale maapizo kuwa ni baraka, kwa vile alivyokupenda Bwana, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 23:6 Deuteronomy 23:6

Usitafute amani yao wala heri yao siku zako zote, milele.

Kumbukumbu la Torati 23:7 Deuteronomy 23:7

Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake.

Kumbukumbu la Torati 23:8 Deuteronomy 23:8

Wana wao watakaozaliwa kizazi cha tatu na waingie katika mkutano wa Bwana.

Kumbukumbu la Torati 23:9 Deuteronomy 23:9

Utakapotoka kwenda juu ya adui zako nawe u katika marago, jilinde na kila neno baya.

Kumbukumbu la Torati 23:10 Deuteronomy 23:10

Akiwa kwenu mtu awaye yote asiyekuwa ni tohara kwa ajili ya yaliyomtukia usiku, na atoke nje ya kituo, wala asiingie ndani ya kituo;

Kumbukumbu la Torati 23:11 Deuteronomy 23:11

lakini na iwe ikaribiapo jioni, yeye ataoga maji; na jua likiisha kuchwa ataingia ndani ya kituo.

Kumbukumbu la Torati 23:12 Deuteronomy 23:12

Tena uwe na mahali nje ya kituo, kwa kutokea nje;

Kumbukumbu la Torati 23:13 Deuteronomy 23:13

nawe uwe na jembe dogo katika silaha zako; napo uotamapo nje uchimbe kwa lile jembe, na kugeuka na kukifunika kikutokacho;

Kumbukumbu la Torati 23:14 Deuteronomy 23:14

kwa kuwa Bwana. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha.

Kumbukumbu la Torati 23:15 Deuteronomy 23:15

Usimrudishe kwa bwana wake mtumwa aliyejiponya kutoka kwa bwana wake kuja kwako;

Kumbukumbu la Torati 23:16 Deuteronomy 23:16

na akae nawe, katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, mahali atakapochagua palipo pema machoni pake; usimwonee.

Kumbukumbu la Torati 23:17 Deuteronomy 23:17

Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume.

Kumbukumbu la Torati 23:18 Deuteronomy 23:18

Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili.

Kumbukumbu la Torati 23:19 Deuteronomy 23:19

Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu cho chote kikopeshwacho kwa riba;

Kumbukumbu la Torati 23:20 Deuteronomy 23:20

mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.

Kumbukumbu la Torati 23:21 Deuteronomy 23:21

Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.

Kumbukumbu la Torati 23:22 Deuteronomy 23:22

Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako.

Kumbukumbu la Torati 23:23 Deuteronomy 23:23

Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri Bwana, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako.

Kumbukumbu la Torati 23:24 Deuteronomy 23:24

Uingiapo katika shamba la mizabibu la jirani yako, utaweza kula zabibu za kukushibisha, kama upendavyo; ila usitie katika chombo chako.

Kumbukumbu la Torati 23:25 Deuteronomy 23:25

Uingiapo katika mmea wa jirani yako waweza kuyapurura masuke kwa mkono wako; ila usisongeze mundu katika mmea wa jirani yako.