Kumbukumbu la Torati Mlango 24 Deuteronomy

Kumbukumbu la Torati 24:1 Deuteronomy 24:1

Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.

Kumbukumbu la Torati 24:2 Deuteronomy 24:2

Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine.

Kumbukumbu la Torati 24:3 Deuteronomy 24:3

Na huyo mumewe wa sasa akimchukia, na kumwandikia hati ya kumwacha, na kumpa mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake; au akifa yeye mumewe wa sasa, aliyemtwaa kuwa mkewe;

Kumbukumbu la Torati 24:4 Deuteronomy 24:4

yule wa kwanza aliyemwacha asimtwae kuwa mkewe tena, akiisha kutiwa unajisi; kwa kuwa haya ni machukizo mbele za Bwana; kwa hiyo usiitie dhambini nchi, akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi.

Kumbukumbu la Torati 24:5 Deuteronomy 24:5

Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yo yote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.

Kumbukumbu la Torati 24:6 Deuteronomy 24:6

Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani.

Kumbukumbu la Torati 24:7 Deuteronomy 24:7

Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwivi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Kumbukumbu la Torati 24:8 Deuteronomy 24:8

Angalia katika pigo la ukoma, utunze kwa bidii, kwa kufanya mfano wa yote watakayowafundisha makuhani Walawi; tunzeni kwa kuyafanya vile vile kama nilivyowaamuru wao.

Kumbukumbu la Torati 24:9 Deuteronomy 24:9

Kumbukeni na Bwana, Mungu wako alivyomtenda Miriamu katika njia mlipotoka Misri.

Kumbukumbu la Torati 24:10 Deuteronomy 24:10

Umkopeshapo jirani yako cho chote kikopeshwacho usiingie katika nyumba yake kwenda kutwaa rehani kwake.

Kumbukumbu la Torati 24:11 Deuteronomy 24:11

Simama nje, yule umkopeshaye akuletee nje ile rehani.

Kumbukumbu la Torati 24:12 Deuteronomy 24:12

Naye akiwa ni mtu maskini, usilale na rehani yake.

Kumbukumbu la Torati 24:13 Deuteronomy 24:13

Sharti umrudishie rehani lichwapo jua, apate kulala na mavazi yake, na kukubarikia; nayo itakuwa ni haki kwako mbele za Bwana, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 24:14 Deuteronomy 24:14

Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako;

Kumbukumbu la Torati 24:15 Deuteronomy 24:15

mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi kwako.

Kumbukumbu la Torati 24:16 Deuteronomy 24:16

Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.

Kumbukumbu la Torati 24:17 Deuteronomy 24:17

Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;

Kumbukumbu la Torati 24:18 Deuteronomy 24:18

bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili.

Kumbukumbu la Torati 24:19 Deuteronomy 24:19

Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili Bwana, Mungu wako, akubariki katika kazi yote ya mikono yako.

Kumbukumbu la Torati 24:20 Deuteronomy 24:20

Utakapochuma matunda ya mizeituni yako, usirudi kuchuma mara ya pili; yaliyobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane.

Kumbukumbu la Torati 24:21 Deuteronomy 24:21

Uchumapo zabibu katika shamba lako la mizabibu, usichume mara ya pili; zilizobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane.

Kumbukumbu la Torati 24:22 Deuteronomy 24:22

Nawe kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili.