Kumbukumbu la Torati Mlango 30 Deuteronomy

Kumbukumbu la Torati 30:1 Deuteronomy 30:1

Tena itakuwa, mambo haya yote yatakapokujilia, baraka na laana nilizoweka mbele yako, nawe utakapozikumbuka kati ya mataifa yote, huko atakakokupeleka Bwana, Mungu wako,

Kumbukumbu la Torati 30:2 Deuteronomy 30:2

nawe utakapomrudia Bwana, Mungu wako, na kuitii sauti yake, mfano wa yote nikuagizayo leo, wewe na wanao, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;

Kumbukumbu la Torati 30:3 Deuteronomy 30:3

ndipo Bwana, Mungu wako, atakapougeuza utumwa wako, naye atakuhurumia, tena atarejea na kukukusanya kutoka mataifa yote, huko alikokutawanyia Bwana, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 30:4 Deuteronomy 30:4

Watu wako waliotawanyika wakiwako katika ncha za mbingu za mwisho, kutoka huko atakukusanya Bwana, Mungu wako; kutoka huko atakutwaa;

Kumbukumbu la Torati 30:5 Deuteronomy 30:5

atakuleta Bwana, Mungu wako, uingie nchi waliyomiliki baba zako, nawe utaimiliki; naye atakutendea mema, na kukufanya uwe watu wengi kuliko baba zako.

Kumbukumbu la Torati 30:6 Deuteronomy 30:6

Bwana, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai.

Kumbukumbu la Torati 30:7 Deuteronomy 30:7

Na laana hizi zote Bwana, Mungu wako, atawatia adui zako na hao wakuchukiao, waliokuwa wakikutesa.

Kumbukumbu la Torati 30:8 Deuteronomy 30:8

Nawe utarudi, uitii sauti ya Bwana, na kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo.

Kumbukumbu la Torati 30:9 Deuteronomy 30:9

Na Bwana, Mungu wako, atakufanya uwe na wingi wa uheri katika kazi yote ya mkono wako, katika uzao wa tumbo lako, na katika uzao wa ng'ombe wako, na katika uzao wa nchi yako; kwa kuwa Bwana atafurahi tena juu yako kwa wema, kama alivyofurahi juu ya baba zako;

Kumbukumbu la Torati 30:10 Deuteronomy 30:10

ukiwa utaifuata sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa kuyashika maagizo yake, na amri zake zilizoandikwa katika chuo hiki cha torati; ukimwelekea Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote.

Kumbukumbu la Torati 30:11 Deuteronomy 30:11

Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali.

Kumbukumbu la Torati 30:12 Deuteronomy 30:12

Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya?

Kumbukumbu la Torati 30:13 Deuteronomy 30:13

Wala si ng'ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya?

Kumbukumbu la Torati 30:14 Deuteronomy 30:14

Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.

Kumbukumbu la Torati 30:15 Deuteronomy 30:15

Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya;

Kumbukumbu la Torati 30:16 Deuteronomy 30:16

kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka; Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki.

Kumbukumbu la Torati 30:17 Deuteronomy 30:17

Lakini moyo wako ukikengeuka, usipotaka kusikiza, lakini ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia;

Kumbukumbu la Torati 30:18 Deuteronomy 30:18

nawahubiri hivi leo hakika mtaangamia; hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi, uivukiayo Yordani, uingie kuimiliki.

Kumbukumbu la Torati 30:19 Deuteronomy 30:19

Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;

Kumbukumbu la Torati 30:20 Deuteronomy 30:20

kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate kukaa katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kuwa atawapa.