Kumbukumbu la Torati Mlango 14 Deuteronomy

Kumbukumbu la Torati 14:1 Deuteronomy 14:1

Ninyi mmekuwa wana wa Bwana, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa.

Kumbukumbu la Torati 14:2 Deuteronomy 14:2

Kwa kuwa u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako, na Bwana amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi.

Kumbukumbu la Torati 14:3 Deuteronomy 14:3

Usile kitu cho chote kichukizacho.

Kumbukumbu la Torati 14:4 Deuteronomy 14:4

Wanyama mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi,

Kumbukumbu la Torati 14:5 Deuteronomy 14:5

kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima;

Kumbukumbu la Torati 14:6 Deuteronomy 14:6

na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla.

Kumbukumbu la Torati 14:7 Deuteronomy 14:7

Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;

Kumbukumbu la Torati 14:8 Deuteronomy 14:8

na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.

Kumbukumbu la Torati 14:9 Deuteronomy 14:9

Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula;

Kumbukumbu la Torati 14:10 Deuteronomy 14:10

na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu.

Kumbukumbu la Torati 14:11 Deuteronomy 14:11

Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.

Kumbukumbu la Torati 14:12 Deuteronomy 14:12

Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu;

Kumbukumbu la Torati 14:13 Deuteronomy 14:13

na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake;

Kumbukumbu la Torati 14:14 Deuteronomy 14:14

na kila kunguru kwa aina zake;

Kumbukumbu la Torati 14:15 Deuteronomy 14:15

na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;

Kumbukumbu la Torati 14:16 Deuteronomy 14:16

na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa;

Kumbukumbu la Torati 14:17 Deuteronomy 14:17

na mwari, na nderi, na mnandi;

Kumbukumbu la Torati 14:18 Deuteronomy 14:18

na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo.

Kumbukumbu la Torati 14:19 Deuteronomy 14:19

Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale.

Kumbukumbu la Torati 14:20 Deuteronomy 14:20

Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.

Kumbukumbu la Torati 14:21 Deuteronomy 14:21

Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.

Kumbukumbu la Torati 14:22 Deuteronomy 14:22

Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

Kumbukumbu la Torati 14:23 Deuteronomy 14:23

Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.

Kumbukumbu la Torati 14:24 Deuteronomy 14:24

Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;

Kumbukumbu la Torati 14:25 Deuteronomy 14:25

ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;

Kumbukumbu la Torati 14:26 Deuteronomy 14:26

na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;

Kumbukumbu la Torati 14:27 Deuteronomy 14:27

na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.

Kumbukumbu la Torati 14:28 Deuteronomy 14:28

Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;

Kumbukumbu la Torati 14:29 Deuteronomy 14:29

na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.