Kumbukumbu la Torati Mlango 1 Deuteronomy

Kumbukumbu la Torati 1:1 Deuteronomy 1:1

Haya ndiyo maneno Musa aliyowaambia Israeli wote ng'ambo ya Yordani barani, katika Araba lililoelekea Sufu, kati ya Parani, na Tofeli, na Labani, na Hazerothi, na Dizahabu.

Kumbukumbu la Torati 1:2 Deuteronomy 1:2

Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya mlima wa Seiri mpaka Kadesh-barnea.

Kumbukumbu la Torati 1:3 Deuteronomy 1:3

Ikawa mwaka wa arobaini, mwezi wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, Musa akawaambia wana wa Israeli kama yote aliyopewa na Bwana ya kuwaamuru;

Kumbukumbu la Torati 1:4 Deuteronomy 1:4

alipokwisha kumpiga Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa akikaa Ashtarothi iliyo katika Edrei;

Kumbukumbu la Torati 1:5 Deuteronomy 1:5

ni ng'ambo ya Yordani katika nchi ya Moabu, alipoanza Musa kufunua torati hii, akisema,

Kumbukumbu la Torati 1:6 Deuteronomy 1:6

Bwana, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu vyatosha;

Kumbukumbu la Torati 1:7 Deuteronomy 1:7

geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima-vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani-pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati.

Kumbukumbu la Torati 1:8 Deuteronomy 1:8

Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi Bwana aliyowaapia baba zenu, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.

Kumbukumbu la Torati 1:9 Deuteronomy 1:9

Nami wakati ule niliwaambia, nikasema, Siwezi mimi mwenyewe kuwachukua peke yangu.

Kumbukumbu la Torati 1:10 Deuteronomy 1:10

Bwana, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi.

Kumbukumbu la Torati 1:11 Deuteronomy 1:11

Bwana, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabarikia, kama alivyowaahidi.

Kumbukumbu la Torati 1:12 Deuteronomy 1:12

Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu, na mzigo wenu, na mateto yenu?

Kumbukumbu la Torati 1:13 Deuteronomy 1:13

Jitwalieni watu wenye akili na fahamu, watu wanaojulikana, kwa kadiri ya kabila zenu, nami nitawafanya wawe vichwa juu yenu.

Kumbukumbu la Torati 1:14 Deuteronomy 1:14

Nanyi mkanijibu, mkaniambia, Jambo ulilonena ni jema la kufanya.

Kumbukumbu la Torati 1:15 Deuteronomy 1:15

Basi nikatwaa vichwa vya kabila zenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe vichwa juu yenu, maakida ya elfu elfu, na maakida ya mia mia, na maakida ya hamsini hamsini, na maakida ya kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya kabila zenu.

Kumbukumbu la Torati 1:16 Deuteronomy 1:16

Nikawaagiza wakati ule waamuzi wenu, nikawaambia, Sikizeni ninyi maneno kati ya ndugu zenu, mkaamue kwa haki kati ya mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye.

Kumbukumbu la Torati 1:17 Deuteronomy 1:17

Msitazame nafsi za watu katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu awaye yote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.

Kumbukumbu la Torati 1:18 Deuteronomy 1:18

Nikawaamuru wakati huo mambo yote yaliyowapasa ninyi kuyafanya.

Kumbukumbu la Torati 1:19 Deuteronomy 1:19

Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama Bwana, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea.

Kumbukumbu la Torati 1:20 Deuteronomy 1:20

Nami nikawaambia, Mmefika nchi ya vilima ya Waamori, anayotupa sisi Bwana, Mungu wetu.

Kumbukumbu la Torati 1:21 Deuteronomy 1:21

Tazama, Bwana, Mungu wako, ameiweka nchi mbele yako; haya panda, itamalaki, kama Bwana, Mungu wa baba zako, alivyokuambia; usiogope wala usifadhaike.

Kumbukumbu la Torati 1:22 Deuteronomy 1:22

Nanyi mkanikaribia kila mmoja wenu, mkasema, Na tupeleke watu mbele yetu, ili watupelelezee nchi na kutuletea habari za njia itupasayo kuipandia, na za miji tutakayoifikia.

Kumbukumbu la Torati 1:23 Deuteronomy 1:23

Neno hili likanipendeza sana; nikatwaa watu kumi na wawili, mtu mmoja wa kila kabila.

Kumbukumbu la Torati 1:24 Deuteronomy 1:24

Nao wakageuka, wakapanda mlimani wakafika bonde la Eshkoli, wakalipeleleza.

Kumbukumbu la Torati 1:25 Deuteronomy 1:25

Wakatwaa baadhi ya matunda ya nchi ile mikononi mwao, wakatuletea huku chini, wakatuletea habari tena, wakasema, Nchi hii anayotupa Bwana, Mungu wetu, ni nchi njema.

Kumbukumbu la Torati 1:26 Deuteronomy 1:26

Lakini hamkukubali kukwea huko, mlihalifu neno la Bwana, Mungu wenu;

Kumbukumbu la Torati 1:27 Deuteronomy 1:27

mkanung'unika hemani mwenu, mkasema, Ni kwa sababu Bwana ametuchukia, ndipo akatutoa katika nchi ya Misri, apate kututia katika mikono ya Waamori, ili kutuangamiza.

Kumbukumbu la Torati 1:28 Deuteronomy 1:28

Twakwea kwenda wapi? Ndugu zetu wameiyeyusha mioyo yetu, wakituambia, Wale watu ni wengi, ni warefu kuliko sisi; miji nayo ni mikubwa, imejengewa kuta hata mbinguni; na zaidi ya hayo huko tumewaona Waanaki.

Kumbukumbu la Torati 1:29 Deuteronomy 1:29

Ndipo nikawaambieni, Msifanye hofu, wala msiwache.

Kumbukumbu la Torati 1:30 Deuteronomy 1:30

Bwana, Mungu wenu, anayetangulia mbele yenu, ndiye atakayewapigania, kwa mfano wa yote aliyowafanyia huko Misri mbele ya macho yenu;

Kumbukumbu la Torati 1:31 Deuteronomy 1:31

na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua Bwana, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafikilia mahali hapa.

Kumbukumbu la Torati 1:32 Deuteronomy 1:32

Lakini katika jambo hili hamkumwamini Bwana, Mungu wenu,

Kumbukumbu la Torati 1:33 Deuteronomy 1:33

aliyewatangulia njiani, usiku kwa moto, kuwaonyesha njia mtakayoiendea, na mchana kwa hilo wingu, ili apate kuwatafutia mahali pa kusimamisha hema zenu.

Kumbukumbu la Torati 1:34 Deuteronomy 1:34

Bwana akaisikia sauti ya maneno yenu, akaghadhibika, akaapa, akasema,

Kumbukumbu la Torati 1:35 Deuteronomy 1:35

Hakika yangu hapana mmoja miongoni mwa watu hawa wa kizazi hiki kibaya atakayeiona nchi hiyo nzuri, niliyowaapia baba zenu kuwapa,

Kumbukumbu la Torati 1:36 Deuteronomy 1:36

isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, huyo ataiona; nami nitampa yeye na watoto wake nchi hiyo aliyoikanyaga; kwa kuwa amemfuata Bwana kwa kila neno.

Kumbukumbu la Torati 1:37 Deuteronomy 1:37

Na Bwana alinikasirikia mimi kwa ajili yenu, akasema, Wala wewe hutaingia humo;

Kumbukumbu la Torati 1:38 Deuteronomy 1:38

Yoshua mwana wa Nuni asimamaye mbele yako ndiye atakayeingia; mtie moyo; kwa kuwa yeye atawarithisha Israeli.

Kumbukumbu la Torati 1:39 Deuteronomy 1:39

Tena, wadogo wenu, mliosema watakuwa mateka, na wana wenu, wasiokuwa leo na maarifa ya mabaya wala mema, ndio watakaoingia, nao ndio nitakaowapa, nao wataimiliki.

Kumbukumbu la Torati 1:40 Deuteronomy 1:40

Na ninyi basi geukeni, mshike safari yenu, mwende jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu.

Kumbukumbu la Torati 1:41 Deuteronomy 1:41

Ndipo mkanijibu, mkaniambia, Sisi tumefanya dhambi juu ya Bwana, tutakwea kupigana kwa mfano wa yote tuliyoamriwa na Bwana. Mkajifunga kila mtu silaha zake za vita, mkafanya wepesi kukwea mlimani.

Kumbukumbu la Torati 1:42 Deuteronomy 1:42

Bwana akaniambia, Uwaambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi si kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu.

Kumbukumbu la Torati 1:43 Deuteronomy 1:43

Basi niliwaambia, msinisikize, bali mliasi amri ya Bwana, mkajikinai, na kukwea mlimani.

Kumbukumbu la Torati 1:44 Deuteronomy 1:44

Na Waamori waliokuwa wakikaa katika mlima huo, waliwatokea juu yenu, wakawafukuza, kama wafukuzwao na nyuki, wakawapomoshea Seiri mpaka Horma.

Kumbukumbu la Torati 1:45 Deuteronomy 1:45

Mkarudi mkalia mbele za Bwana; Bwana asiisikize sauti yenu, wala hakuelekeza masikio yake kwenu.

Kumbukumbu la Torati 1:46 Deuteronomy 1:46

Ndipo mkakaa Kadeshi siku nyingi, kwa kadiri ya hizo siku mlizokaa.