Kumbukumbu la Torati Mlango 34 Deuteronomy

Kumbukumbu la Torati 34:1 Deuteronomy 34:1

Musa akapanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo, hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko. Bwana akamwonyesha nchi yote ya Gileadi hata Dani;

Kumbukumbu la Torati 34:2 Deuteronomy 34:2

na Naftali yote, na nchi ya Efraimu na Manase, na nchi yote ya Yuda, mpaka bahari ya magharibi;

Kumbukumbu la Torati 34:3 Deuteronomy 34:3

na Negebu, na uwanja wa bonde la Yeriko, mji wa mitende, hata mpaka Soari.

Kumbukumbu la Torati 34:4 Deuteronomy 34:4

Bwana akamwambia, Hii ndiyo nchi niliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, nikisema, Nitawapa wazao wako. Basi nimekuonyesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko.

Kumbukumbu la Torati 34:5 Deuteronomy 34:5

Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la Bwana.

Kumbukumbu la Torati 34:6 Deuteronomy 34:6

Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo.

Kumbukumbu la Torati 34:7 Deuteronomy 34:7

Musa alikuwa mtu wa miaka mia na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka.

Kumbukumbu la Torati 34:8 Deuteronomy 34:8

Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha.

Kumbukumbu la Torati 34:9 Deuteronomy 34:9

Na Yoshua, mwana wa Nuni, alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake; wana wa Israeli wakamsikiliza, wakafanya kama Bwana alivyomwamuru Musa.

Kumbukumbu la Torati 34:10 Deuteronomy 34:10

Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso;

Kumbukumbu la Torati 34:11 Deuteronomy 34:11

katika ishara zote na maajabu yote, ambayo Bwana alimtuma kuyatenda katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote;

Kumbukumbu la Torati 34:12 Deuteronomy 34:12

na katika ule mkono wa nguvu wote, tena katika ule utisho mkuu wote, alioutenda Musa machoni pa Israeli wote.