Kumbukumbu la Torati Mlango 18 Deuteronomy

Kumbukumbu la Torati 18:1 Deuteronomy 18:1

Makuhani Walawi, kabila yote ya Lawi, wasiwe na fungu wala urithi pamoja na Israeli; watakula sadaka za Bwana zifanywazo kwa moto, na urithi wake.

Kumbukumbu la Torati 18:2 Deuteronomy 18:2

Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.

Kumbukumbu la Torati 18:3 Deuteronomy 18:3

Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na tumbo.

Kumbukumbu la Torati 18:4 Deuteronomy 18:4

Malimbuko ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, umpe.

Kumbukumbu la Torati 18:5 Deuteronomy 18:5

Kwani Bwana, Mungu wako, amemchagua katika kabila zako zote, asimame atumike kwa jina la Bwana, yeye na wanawe milele.

Kumbukumbu la Torati 18:6 Deuteronomy 18:6

Na akija Mlawi atokaye katika malango yako mojawapo, katika Israeli yote alipokuwa akikaa, akaja kwa mapenzi yote ya nafsi yake mahali atakapochagua Bwana;

Kumbukumbu la Torati 18:7 Deuteronomy 18:7

na atumike kwa jina la Bwana, Mungu wake, kama wafanyavyo ndugu zake wote, Walawi wasimamao huko mbele za Bwana.

Kumbukumbu la Torati 18:8 Deuteronomy 18:8

Wawe na fungu sawasawa la kula, pamoja na haya yaliyomfikilia kwa kuuzwa urithi wa baba zake.

Kumbukumbu la Torati 18:9 Deuteronomy 18:9

Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale.

Kumbukumbu la Torati 18:10 Deuteronomy 18:10

Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

Kumbukumbu la Torati 18:11 Deuteronomy 18:11

wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

Kumbukumbu la Torati 18:12 Deuteronomy 18:12

Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.

Kumbukumbu la Torati 18:13 Deuteronomy 18:13

Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 18:14 Deuteronomy 18:14

Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo.

Kumbukumbu la Torati 18:15 Deuteronomy 18:15

Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.

Kumbukumbu la Torati 18:16 Deuteronomy 18:16

Kama vile ulivyotaka kwa Bwana, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya Bwana, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa.

Kumbukumbu la Torati 18:17 Deuteronomy 18:17

Bwana akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema.

Kumbukumbu la Torati 18:18 Deuteronomy 18:18

Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.

Kumbukumbu la Torati 18:19 Deuteronomy 18:19

Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake.

Kumbukumbu la Torati 18:20 Deuteronomy 18:20

Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.

Kumbukumbu la Torati 18:21 Deuteronomy 18:21

Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena Bwana?

Kumbukumbu la Torati 18:22 Deuteronomy 18:22

Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope