Mithali Mlango 20 Proverbs

Mithali 20:1 Proverbs 20:1

Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.

Mithali 20:2 Proverbs 20:2

Utisho wa mfalme ni kama ngurumo ya simba; Amkasirishaye huitendea dhambi nafsi yake.

Mithali 20:3 Proverbs 20:3

Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana.

Mithali 20:4 Proverbs 20:4

Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.

Mithali 20:5 Proverbs 20:5

Mashauri ya moyoni ni kama kilindi; Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka.

Mithali 20:6 Proverbs 20:6

Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?

Mithali 20:7 Proverbs 20:7

Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, Watoto wake wabarikiwa baada yake.

Mithali 20:8 Proverbs 20:8

Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu, Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake.

Mithali 20:9 Proverbs 20:9

Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu; Nimetakasika dhambi yangu?

Mithali 20:10 Proverbs 20:10

Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa Bwana.

Mithali 20:11 Proverbs 20:11

Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.

Mithali 20:12 Proverbs 20:12

Sikio lisikialo, na jicho lionalo, Bwana ndiye aliyeyafanya yote mawili.

Mithali 20:13 Proverbs 20:13

Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.

Mithali 20:14 Proverbs 20:14

Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi; Lakini akiisha kwenda zake hujisifu.

Mithali 20:15 Proverbs 20:15

Dhahabu iko, na marijani tele; Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani.

Mithali 20:16 Proverbs 20:16

Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni; Mtoze rehani aliye mdhamini wa wageni.

Mithali 20:17 Proverbs 20:17

Chakula cha uongo ni kitamu kwa mtu; Lakini halafu kinywa chake kitajaa changarawe.

Mithali 20:18 Proverbs 20:18

Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita.

Mithali 20:19 Proverbs 20:19

Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.

Mithali 20:20 Proverbs 20:20

Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu.

Mithali 20:21 Proverbs 20:21

Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka, Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa.

Mithali 20:22 Proverbs 20:22

Usiseme, Mimi nitalipa mabaya; Mngojee Bwana, naye atakuokoa.

Mithali 20:23 Proverbs 20:23

Vipimo mbalimbali ni chukizo kwa Bwana; Tena mizani ya hila si njema.

Mithali 20:24 Proverbs 20:24

Mwenendo wa mtu watoka kwa Bwana; Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake?

Mithali 20:25 Proverbs 20:25

Ni mtego, mtu aseme kwa haraka, Kitu hiki ni wakfu; Na baada ya kuweka nadhiri kuuliza-uliza habari.

Mithali 20:26 Proverbs 20:26

Mfalme mwenye hekima huwapepeta wasio haki; Naye hulipitisha gurudumo la kupuria juu yao.

Mithali 20:27 Proverbs 20:27

Pumzi ya mwanadamu ni taa ya Bwana; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake.

Mithali 20:28 Proverbs 20:28

Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme, Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili.

Mithali 20:29 Proverbs 20:29

Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.

Mithali 20:30 Proverbs 20:30

Machubuko ya fimbo husafisha uovu, Na mapigo hufikilia ndani ya mtima.