Mithali Mlango 18 Proverbs

Mithali 18:1 Proverbs 18:1

Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe; Hushindana na kila shauri jema.

Mithali 18:2 Proverbs 18:2

Mpumbavu hapendezwi na ufahamu; Ila moyo wake udhihirike tu.

Mithali 18:3 Proverbs 18:3

Ajapo asiye haki, huja dharau pia; Na pamoja na aibu huja lawama.

Mithali 18:4 Proverbs 18:4

Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi; Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.

Mithali 18:5 Proverbs 18:5

Kukubali uso wake asiye haki si vizuri; Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.

Mithali 18:6 Proverbs 18:6

Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina, Na kinywa chake huita mapigo.

Mithali 18:7 Proverbs 18:7

Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake, Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.

Mithali 18:8 Proverbs 18:8

Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo; Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.

Mithali 18:9 Proverbs 18:9

Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu.

Mithali 18:10 Proverbs 18:10

Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.

Mithali 18:11 Proverbs 18:11

Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu; Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.

Mithali 18:12 Proverbs 18:12

Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Mithali 18:13 Proverbs 18:13

Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.

Mithali 18:14 Proverbs 18:14

Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake; Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?

Mithali 18:15 Proverbs 18:15

Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.

Mithali 18:16 Proverbs 18:16

Zawadi ya mtu humpatia nafasi; Humleta mbele ya watu wakuu.

Mithali 18:17 Proverbs 18:17

Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki; Lakini jirani yake huja na kumchunguza.

Mithali 18:18 Proverbs 18:18

Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.

Mithali 18:19 Proverbs 18:19

Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.

Mithali 18:20 Proverbs 18:20

Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.

Mithali 18:21 Proverbs 18:21

Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.

Mithali 18:22 Proverbs 18:22

Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.

Mithali 18:23 Proverbs 18:23

Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali.

Mithali 18:24 Proverbs 18:24

Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.