Mithali Mlango 23 Proverbs

Mithali 23:1 Proverbs 23:1

Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala, Mwangalie sana yeye aliye mbele yako.

Mithali 23:2 Proverbs 23:2

Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi.

Mithali 23:3 Proverbs 23:3

Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila.

Mithali 23:4 Proverbs 23:4

Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.

Mithali 23:5 Proverbs 23:5

Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni.

Mithali 23:6 Proverbs 23:6

Usile mkate wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa;

Mithali 23:7 Proverbs 23:7

Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.

Mithali 23:8 Proverbs 23:8

Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea.

Mithali 23:9 Proverbs 23:9

Usiseme masikioni mwa mpumbavu; Maana atadharau hekima ya maneno yako.

Mithali 23:10 Proverbs 23:10

Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani; Wala usiingie katika mashamba ya yatima;

Mithali 23:11 Proverbs 23:11

Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako.

Mithali 23:12 Proverbs 23:12

Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.

Mithali 23:13 Proverbs 23:13

Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

Mithali 23:14 Proverbs 23:14

Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.

Mithali 23:15 Proverbs 23:15

Mwanangu, kama moyo wako una hekima, Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu;

Mithali 23:16 Proverbs 23:16

Naam, viuno vyangu vitafurahi, Midomo yako inenapo maneno mema.

Mithali 23:17 Proverbs 23:17

Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche Bwana mchana kutwa;

Mithali 23:18 Proverbs 23:18

Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika.

Mithali 23:19 Proverbs 23:19

Sikia, mwanangu, uwe na hekima, Na kuuongoza moyo wako katika njia njema.

Mithali 23:20 Proverbs 23:20

Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.

Mithali 23:21 Proverbs 23:21

Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.

Mithali 23:22 Proverbs 23:22

Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.

Mithali 23:23 Proverbs 23:23

Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu.

Mithali 23:24 Proverbs 23:24

Baba yake mwenye haki atashangilia; Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia.

Mithali 23:25 Proverbs 23:25

Na wafurahi baba yako na mama yako; Na afurahi aliyekuzaa.

Mithali 23:26 Proverbs 23:26

Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu.

Mithali 23:27 Proverbs 23:27

Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba.

Mithali 23:28 Proverbs 23:28

Naam, huotea kama mnyang'anyi; Huwaongeza wenye hila katika wanadamu.

Mithali 23:29 Proverbs 23:29

Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?

Mithali 23:30 Proverbs 23:30

Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.

Mithali 23:31 Proverbs 23:31

Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;

Mithali 23:32 Proverbs 23:32

Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.

Mithali 23:33 Proverbs 23:33

Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.

Mithali 23:34 Proverbs 23:34

Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.

Mithali 23:35 Proverbs 23:35

Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.