Mithali Mlango 31 Proverbs

Mithali 31:1 Proverbs 31:1

Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.

Mithali 31:2 Proverbs 31:2

Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?

Mithali 31:3 Proverbs 31:3

Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.

Mithali 31:4 Proverbs 31:4

Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?

Mithali 31:5 Proverbs 31:5

Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.

Mithali 31:6 Proverbs 31:6

Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.

Mithali 31:7 Proverbs 31:7

Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.

Mithali 31:8 Proverbs 31:8

Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao;

Mithali 31:9 Proverbs 31:9

Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie maskini na wahitaji haki yao.

Mithali 31:10 Proverbs 31:10

Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.

Mithali 31:11 Proverbs 31:11

Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.

Mithali 31:12 Proverbs 31:12

Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.

Mithali 31:13 Proverbs 31:13

Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.

Mithali 31:14 Proverbs 31:14

Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.

Mithali 31:15 Proverbs 31:15

Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.

Mithali 31:16 Proverbs 31:16

Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.

Mithali 31:17 Proverbs 31:17

Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.

Mithali 31:18 Proverbs 31:18

Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.

Mithali 31:19 Proverbs 31:19

Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.

Mithali 31:20 Proverbs 31:20

Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.

Mithali 31:21 Proverbs 31:21

Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.

Mithali 31:22 Proverbs 31:22

Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.

Mithali 31:23 Proverbs 31:23

Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.

Mithali 31:24 Proverbs 31:24

Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.

Mithali 31:25 Proverbs 31:25

Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.

Mithali 31:26 Proverbs 31:26

Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.

Mithali 31:27 Proverbs 31:27

Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.

Mithali 31:28 Proverbs 31:28

Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,

Mithali 31:29 Proverbs 31:29

Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.

Mithali 31:30 Proverbs 31:30

Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.

Mithali 31:31 Proverbs 31:31

Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.