Mithali Mlango 14 Proverbs

Mithali 14:1 Proverbs 14:1

Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Mithali 14:2 Proverbs 14:2

Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha Bwana; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau.

Mithali 14:3 Proverbs 14:3

Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi.

Mithali 14:4 Proverbs 14:4

Zizi ni safi ambapo hapana ng'ombe; Bali nguvu za ng'ombe zaleta faida nyingi.

Mithali 14:5 Proverbs 14:5

Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.

Mithali 14:6 Proverbs 14:6

Mwenye dharau hutafuta hekima, asiipate; Bali maarifa huwa mepesi kwa mwenye ufahamu.

Mithali 14:7 Proverbs 14:7

Toka mbele ya uso wa mpumbavu, Maana hutaona kwake midomo ya maarifa.

Mithali 14:8 Proverbs 14:8

Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.

Mithali 14:9 Proverbs 14:9

Wapumbavu huidharau hatia; Bali upo upendeleo kwa wenye haki.

Mithali 14:10 Proverbs 14:10

Moyo huujua uchungu wa nafsi yake, Wala mgeni haishiriki furaha yake.

Mithali 14:11 Proverbs 14:11

Nyumba ya mtu mbaya itabomolewa; Bali hema ya mwenye haki itafanikiwa.

Mithali 14:12 Proverbs 14:12

Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

Mithali 14:13 Proverbs 14:13

Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.

Mithali 14:14 Proverbs 14:14

Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe; Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake.

Mithali 14:15 Proverbs 14:15

Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo.

Mithali 14:16 Proverbs 14:16

Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu; Bali mpumbavu ana ufidhuli, na kujitumai.

Mithali 14:17 Proverbs 14:17

Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa.

Mithali 14:18 Proverbs 14:18

Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji ya maarifa.

Mithali 14:19 Proverbs 14:19

Wabaya huinama mbele ya wema, Na wasio haki malangoni mwao wenye haki.

Mithali 14:20 Proverbs 14:20

Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi.

Mithali 14:21 Proverbs 14:21

Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri.

Mithali 14:22 Proverbs 14:22

Je! Hawakosi wawazao mabaya? Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema.

Mithali 14:23 Proverbs 14:23

Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.

Mithali 14:24 Proverbs 14:24

Taji ya wenye hekima ni mali zao; Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu.

Mithali 14:25 Proverbs 14:25

Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu; Bali atoaye uongo hudanganya.

Mithali 14:26 Proverbs 14:26

Kumcha Bwana ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio.

Mithali 14:27 Proverbs 14:27

Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.

Mithali 14:28 Proverbs 14:28

Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao.

Mithali 14:29 Proverbs 14:29

Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.

Mithali 14:30 Proverbs 14:30

Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa.

Mithali 14:31 Proverbs 14:31

Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu.

Mithali 14:32 Proverbs 14:32

Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.

Mithali 14:33 Proverbs 14:33

Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu; Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika.

Mithali 14:34 Proverbs 14:34

Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.

Mithali 14:35 Proverbs 14:35

Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.