Mithali Mlango 6 Proverbs

Mithali 6:1 Proverbs 6:1

Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa rafiki yako, Ikiwa wewe na mgeni mmepana mikono,

Mithali 6:2 Proverbs 6:2

Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,

Mithali 6:3 Proverbs 6:3

Sasa, mwanangu, fanya hivi ukajiokoe, Kwa kuwa umejitia mkononi mwa jirani yako; Nenda ukanyenyekee, na kumsihi jirani yako.

Mithali 6:4 Proverbs 6:4

Usiache macho yako kupata usingizi, Wala kope za macho yako kusinzia.

Mithali 6:5 Proverbs 6:5

Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego.

Mithali 6:6 Proverbs 6:6

Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.

Mithali 6:7 Proverbs 6:7

Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu,

Mithali 6:8 Proverbs 6:8

Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

Mithali 6:9 Proverbs 6:9

Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?

Mithali 6:10 Proverbs 6:10

Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!

Mithali 6:11 Proverbs 6:11

Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

Mithali 6:12 Proverbs 6:12

Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu.

Mithali 6:13 Proverbs 6:13

Hukonyeza kwa macho, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake.

Mithali 6:14 Proverbs 6:14

Mna upotofu moyoni mwake, hutunga uovu daima, Hupanda mbegu za magomvi.

Mithali 6:15 Proverbs 6:15

Basi msiba utampata kwa ghafula; Ghafula atavunjika, bila njia ya kupona.

Mithali 6:16 Proverbs 6:16

Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.

Mithali 6:17 Proverbs 6:17

Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;

Mithali 6:18 Proverbs 6:18

Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;

Mithali 6:19 Proverbs 6:19

Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

Mithali 6:20 Proverbs 6:20

Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako.

Mithali 6:21 Proverbs 6:21

Yafunge hayo katika moyo wako daima; Jivike hayo shingoni mwako.

Mithali 6:22 Proverbs 6:22

Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda, Na uamkapo yatazungumza nawe.

Mithali 6:23 Proverbs 6:23

Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru, Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.

Mithali 6:24 Proverbs 6:24

Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.

Mithali 6:25 Proverbs 6:25

Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.

Mithali 6:26 Proverbs 6:26

Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani

Mithali 6:27 Proverbs 6:27

Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketezwe?

Mithali 6:28 Proverbs 6:28

Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue?

Mithali 6:29 Proverbs 6:29

Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.

Mithali 6:30 Proverbs 6:30

Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa;

Mithali 6:31 Proverbs 6:31

Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake.

Mithali 6:32 Proverbs 6:32

Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

Mithali 6:33 Proverbs 6:33

Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.

Mithali 6:34 Proverbs 6:34

Maana wivu ni ghadhabu ya mtu; Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi.

Mithali 6:35 Proverbs 6:35

Hatakubali ukombozi uwao wote; Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi.