Kutoka Mlango 1 Exodus

Kutoka 1:1 Exodus 1:1

Basi majina ya wana wa Israeli walioingia Misri ni haya; kila mtu pamoja na jamaa zake walikuja pamoja na Yakobo.

Kutoka 1:2 Exodus 1:2

Reubeni, na Simeoni na Lawi, na Yuda;

Kutoka 1:3 Exodus 1:3

na Isakari, na Zabuloni, na Benyamini;

Kutoka 1:4 Exodus 1:4

na Dani, na Naftali, na Gadi, na Asheri.

Kutoka 1:5 Exodus 1:5

Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo.

Kutoka 1:6 Exodus 1:6

Yusufu akafa, na ndugu zake wote, na watu wote wa kizazi kile.

Kutoka 1:7 Exodus 1:7

Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.

Kutoka 1:8 Exodus 1:8

Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.

Kutoka 1:9 Exodus 1:9

Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.

Kutoka 1:10 Exodus 1:10

Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.

Kutoka 1:11 Exodus 1:11

Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.

Kutoka 1:12 Exodus 1:12

Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli.

Kutoka 1:13 Exodus 1:13

Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali;

Kutoka 1:14 Exodus 1:14

wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.

Kutoka 1:15 Exodus 1:15

Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua;

Kutoka 1:16 Exodus 1:16

akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.

Kutoka 1:17 Exodus 1:17

Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.

Kutoka 1:18 Exodus 1:18

Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai?

Kutoka 1:19 Exodus 1:19

Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.

Kutoka 1:20 Exodus 1:20

Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi.

Kutoka 1:21 Exodus 1:21

Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.

Kutoka 1:22 Exodus 1:22

Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.