Kutoka Mlango 23 Exodus

Kutoka 23:1 Exodus 23:1

Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu.

Kutoka 23:2 Exodus 23:2

Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;

Kutoka 23:3 Exodus 23:3

wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake.

Kutoka 23:4 Exodus 23:4

Ukimwona ng'ombe wa adui wako, au punda wake, amepotea, sharti umrudishie mwenyewe tena.

Kutoka 23:5 Exodus 23:5

Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye hali ameanguka chini ya mzigo wake, nawe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.

Kutoka 23:6 Exodus 23:6

Usipotoe hukumu ya mtu maskini katika neno lake.

Kutoka 23:7 Exodus 23:7

Jitenge mbali na neno uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu.

Kutoka 23:8 Exodus 23:8

Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki.

Kutoka 23:9 Exodus 23:9

Usimwonee mgeni; maana, ninyi mwajua moyo wa mgeni ulivyo, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.

Kutoka 23:10 Exodus 23:10

Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake;

Kutoka 23:11 Exodus 23:11

lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni.

Kutoka 23:12 Exodus 23:12

Siku sita utafanya kazi yako, na siku ya saba utapumzika; ili kwamba ng'ombe wako na punda wako wapate kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako na mgeni wapate kuburudika.

Kutoka 23:13 Exodus 23:13

Yaangalieni hayo yote niliyowaambia; wala msitaje kabisa majina ya miungu mingine, wala yasisikizwe kutoka kinywani mwako.

Kutoka 23:14 Exodus 23:14

Mara tatu kila mwaka utaniwekea sikukuu.

Kutoka 23:15 Exodus 23:15

Utaiweka sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu; utakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba kama nilivyokuagiza, kwa wakati uliowekwa, mwezi wa Abibu (kwa maana ndio mwezi uliotoka Misri); wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu;

Kutoka 23:16 Exodus 23:16

tena, sikukuu ya mavuno, hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani.

Kutoka 23:17 Exodus 23:17

Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU.

Kutoka 23:18 Exodus 23:18

Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi.

Kutoka 23:19 Exodus 23:19

Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Kutoka 23:20 Exodus 23:20

Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.

Kutoka 23:21 Exodus 23:21

Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake.

Kutoka 23:22 Exodus 23:22

Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.

Kutoka 23:23 Exodus 23:23

Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali.

Kutoka 23:24 Exodus 23:24

Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande.

Kutoka 23:25 Exodus 23:25

Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.

Kutoka 23:26 Exodus 23:26

Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.

Kutoka 23:27 Exodus 23:27

Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao.

Kutoka 23:28 Exodus 23:28

Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako.

Kutoka 23:29 Exodus 23:29

Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua.

Kutoka 23:30 Exodus 23:30

Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi.

Kutoka 23:31 Exodus 23:31

Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hata bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako.

Kutoka 23:32 Exodus 23:32

Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao.

Kutoka 23:33 Exodus 23:33

Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni tanzi kwako.