Kutoka Mlango 40 Exodus

Kutoka 40:1 Exodus 40:1

Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

Kutoka 40:2 Exodus 40:2

Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza utaisimamisha hiyo maskani ya hema ya kukutania.

Kutoka 40:3 Exodus 40:3

Nawe utatia ndani yake sanduku la ushuhuda, nawe utalisitiri hilo sanduku kwa pazia.

Kutoka 40:4 Exodus 40:4

Nawe utaleta meza na kuitia ndani, na kuviweka sawasawa vile vitu juu yake; kisha utakileta ndani kile kinara cha taa, na kuziwasha taa zake.

Kutoka 40:5 Exodus 40:5

Kisha utaisimamisha madhabahu ya dhahabu kwa kufukizia uvumba mbele ya sanduku la ushuhuda, na kulitia pazia mlangoni mwa hiyo maskani.

Kutoka 40:6 Exodus 40:6

Kisha utaweka madhabahu ya kuteketeza sadaka mbele ya mlango wa maskani ya hema ya kukutania.

Kutoka 40:7 Exodus 40:7

Kisha utaliweka birika kati ya hema ya kukutania na hiyo madhabahu, nawe utatia maji ndani yake.

Kutoka 40:8 Exodus 40:8

Kisha utausimamisha ukuta wa ua kuuzunguka pande zote, na kuitundika sitara ya lango la ua.

Kutoka 40:9 Exodus 40:9

Kisha utayatwaa mafuta ya kutiwa, na kuitia mafuta hiyo maskani, na kila kitu kilicho ndani yake, na kuiweka iwe takatifu, na vyombo vyake vyote; nayo itakuwa takatifu.

Kutoka 40:10 Exodus 40:10

Kisha utaitia mafuta madhabahu ya kuteketeza sadaka, na vyombo vyake vyote; na kuiweka takatifu madhabahu; na hiyo madhabahu itakuwa takatifu sana.

Kutoka 40:11 Exodus 40:11

Kisha utalitia mafuta birika na tako lake, na kuliweka liwe takatifu.

Kutoka 40:12 Exodus 40:12

Kisha utamleta Haruni na wanawe hapo mlangoni pa hema ya kukutania, nawe utawaosha kwa maji.

Kutoka 40:13 Exodus 40:13

Kisha utamvika Haruni mavazi matakatifu; nawe utamtia mafuta, na kumweka awe mtakatifu, ili apate kunitumikia katika kazi ya ukuhani.

Kutoka 40:14 Exodus 40:14

Kisha utawaleta wanawe, na kuwavika kanzu zao;

Kutoka 40:15 Exodus 40:15

nawe utawatia mafuta kama ulivyomtia mafuta baba yao, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani; na huko kutiwa mafuta kwao kutakuwa ni kwa ukuhani wa milele katika vizazi vyao vyote.

Kutoka 40:16 Exodus 40:16

Musa akafanya hayo yote; kama yote Bwana aliyoagiza ndivyo alivyofanya.

Kutoka 40:17 Exodus 40:17

Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, siku ya kwanza ya mwezi ile maskani ilisimamishwa.

Kutoka 40:18 Exodus 40:18

Musa akaisimamisha maskani, akayaweka matako yake, akazisimamisha mbao zake akayatia mataruma yake, akazisimamisha nguzo zake.

Kutoka 40:19 Exodus 40:19

Akaitanda hema juu ya maskani, akakitia kifuniko cha hema juu yake; kama Bwana alivyomwamuru Musa.

Kutoka 40:20 Exodus 40:20

Akautwaa ule ushuhuda, akautia ndani ya sanduku, akaiweka miti ya kuchukulia juu ya sanduku, akakiweka kiti cha rehema juu ya sanduku;

Kutoka 40:21 Exodus 40:21

kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama Bwana alivyomwamuru Musa.

Kutoka 40:22 Exodus 40:22

Akaitia meza ndani ya hema ya kukutania, upande wa maskani ulioelekea kaskazini, nje ya pazia.

Kutoka 40:23 Exodus 40:23

Akaipanga ile mikate juu yake mbele za Bwana; kama Bwana alivyomwamuru Musa.

Kutoka 40:24 Exodus 40:24

Kisha akakitia kinara cha taa ndani ya hema ya kukutania, kuikabili ile meza, upande wa maskani ulioelekea kusini.

Kutoka 40:25 Exodus 40:25

Kisha akaziwasha taa zake mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwamuru Musa.

Kutoka 40:26 Exodus 40:26

Akaitia madhabahu ya dhahabu ndani ya hema ya kukutania mbele ya pazia.

Kutoka 40:27 Exodus 40:27

Akafukiza juu yake uvumba wa manukato kama Bwana alivyomwamuru Musa.

Kutoka 40:28 Exodus 40:28

Akalitia pazia la mlango wa maskani.

Kutoka 40:29 Exodus 40:29

Akaiweka madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mlangoni pa maskani ya kukutania, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake, na sadaka ya unga; kama Bwana alivyomwamuru Musa.

Kutoka 40:30 Exodus 40:30

Akaliweka birika kati ya hema ya kukutania na madhabahu, akatia maji ndani yake ya kuoshea.

Kutoka 40:31 Exodus 40:31

Musa na Haruni, na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yake;

Kutoka 40:32 Exodus 40:32

hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu walinawa kama Bwana alivyomwamuru Musa.

Kutoka 40:33 Exodus 40:33

Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.

Kutoka 40:34 Exodus 40:34

Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.

Kutoka 40:35 Exodus 40:35

Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.

Kutoka 40:36 Exodus 40:36

Na hapo lile wingu lilipoinuliwa kutoka juu ya maskani, wana wa Israeli wakaenda mbele katika safari zao zote,

Kutoka 40:37 Exodus 40:37

bali kama lile wingu halikuinuliwa, wakati ule hawakusafiri hata siku ile lilipoinuliwa tena.

Kutoka 40:38 Exodus 40:38

Kwa maana lile wingu la Bwana lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.