Kutoka Mlango 31 Exodus

Kutoka 31:1 Exodus 31:1

Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

Kutoka 31:2 Exodus 31:2

Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;

Kutoka 31:3 Exodus 31:3

nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,

Kutoka 31:4 Exodus 31:4

ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba,

Kutoka 31:5 Exodus 31:5

na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.

Kutoka 31:6 Exodus 31:6

Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza;

Kutoka 31:7 Exodus 31:7

yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema;

Kutoka 31:8 Exodus 31:8

na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu ya kufukizia uvumba;

Kutoka 31:9 Exodus 31:9

na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake;

Kutoka 31:10 Exodus 31:10

na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani;

Kutoka 31:11 Exodus 31:11

na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.

Kutoka 31:12 Exodus 31:12

Bwana akasema na Musa, na kumwambia,

Kutoka 31:13 Exodus 31:13

Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.

Kutoka 31:14 Exodus 31:14

Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.

Kutoka 31:15 Exodus 31:15

Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa Bwana; kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato, hakika yake atauawa.

Kutoka 31:16 Exodus 31:16

Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele.

Kutoka 31:17 Exodus 31:17

Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.

Kutoka 31:18 Exodus 31:18

Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.