Kutoka Mlango 21 Exodus

Kutoka 21:1 Exodus 21:1

Basi hukumu utakazoziweka mbele ya watu ni hizi

Kutoka 21:2 Exodus 21:2

Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure.

Kutoka 21:3 Exodus 21:3

Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye.

Kutoka 21:4 Exodus 21:4

Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.

Kutoka 21:5 Exodus 21:5

Lakini huyo mtumwa akisema waziwazi, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; sitaki mimi kutoka niwe huru;

Kutoka 21:6 Exodus 21:6

ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake atalitoboa sikio lake kwa uma; ndipo atamtumikia sikuzote.

Kutoka 21:7 Exodus 21:7

Mtu akimwuza binti yake awe kijakazi, hatatoka yeye kama watumwa wa kiume watokavyo.

Kutoka 21:8 Exodus 21:8

Kwamba bwana wake hakupendezewa naye, akiwa amemposa, ndipo atakubali akombolewe; hana amri yeye kumwuza aende kwa watu wageni maana amemtenda kwa udanganyifu.

Kutoka 21:9 Exodus 21:9

Kwamba amposa mwanawe, atamtendea kama desturi zipasazo binti zake.

Kutoka 21:10 Exodus 21:10

Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.

Kutoka 21:11 Exodus 21:11

Kwamba hamfanyii mambo haya matatu, ndipo atatoka aende bure, pasipo kutolewa mali.

Kutoka 21:12 Exodus 21:12

Mtu awaye yote ampigaye mtu, hata akafa, hana budi atauawa huyo.

Kutoka 21:13 Exodus 21:13

Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonyesha mahali atakapopakimbilia.

Kutoka 21:14 Exodus 21:14

Lakini, mtu akimwendea mwenziwe kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata madhabahuni pangu, auawe.

Kutoka 21:15 Exodus 21:15

Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.

Kutoka 21:16 Exodus 21:16

Yeye amwibaye mtu, na kumwuza, au akipatikana mkononi mwake, sharti atauawa huyo

Kutoka 21:17 Exodus 21:17

Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.

Kutoka 21:18 Exodus 21:18

Watu wakigombana, na mmoja akimpiga mwenziwe kwa jiwe, au kwa konde, asife, lakini yualazwa kitandani mwake;

Kutoka 21:19 Exodus 21:19

atakapoinuka tena na kuenenda nje kwa kutegemea fimbo, ndipo hapo yule aliyempiga ataachwa; ila atamlipa kwa ajili ya hayo majira yake yaliyompotea, naye atamwuguza hata apone kabisa.

Kutoka 21:20 Exodus 21:20

Mtu akimpiga mtumwa wake, au kijakazi chake, kwa fimbo, naye akifa mkononi mwake, hana budi ataadhibiwa.

Kutoka 21:21 Exodus 21:21

Lakini akipona siku moja au mbili hataadhibiwa; maana, ni mali yake.

Kutoka 21:22 Exodus 21:22

Watu waume wakiteta pamoja, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema.

Kutoka 21:23 Exodus 21:23

Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza uhai kwa uhai,

Kutoka 21:24 Exodus 21:24

jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,

Kutoka 21:25 Exodus 21:25

kuteketeza kwa kuteketeza, jeraha kwa jeraha, chubuko kwa ajili ya chubuko.

Kutoka 21:26 Exodus 21:26

Mtu akimpiga mtumwa wake jicho, au jicho la kijakazi chake, na kuliharibu; atamwacha huru kwa ajili ya jicho lake.

Kutoka 21:27 Exodus 21:27

Au akimpiga mtumwa wake jino likang'oka, au jino la kijakazi chake, atamwacha huru kwa ajili ya jino lake.

Kutoka 21:28 Exodus 21:28

Ng'ombe akipiga pembe mtu mume au mtu mke, nao wakafa, huyo ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, nyama yake isiliwe; lakini mwenye huyo ng'ombe ataachiliwa.

Kutoka 21:29 Exodus 21:29

Lakini kwamba huyo ng'ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameonyeshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mtu mume au mwanamke; huyo ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa.

Kutoka 21:30 Exodus 21:30

Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa.

Kutoka 21:31 Exodus 21:31

Akiwa ng'ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa kama hukumu hiyo.

Kutoka 21:32 Exodus 21:32

Ng'ombe akimtumbua mtumwa mume au kijakazi; mwenye ng'ombe atampa bwana wao shekeli thelathini za fedha, naye ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe.

Kutoka 21:33 Exodus 21:33

Kwamba mtu atafunua shimo, au kuchimba shimo, naye asilifunike, kisha ikawa ng'ombe au punda kutumbukia humo,

Kutoka 21:34 Exodus 21:34

mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake.

Kutoka 21:35 Exodus 21:35

Ng'ombe wa mtu akimwumiza ng'ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza huyo ng'ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng'ombe aliyekufa pia watamgawanya.

Kutoka 21:36 Exodus 21:36

Au kwamba ilijulikana ya kuwa ng'ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng'ombe kwa ng'ombe, na huyo ng'ombe aliyekufa atakuwa ni wake.