Kutoka Mlango 25 Exodus

Kutoka 25:1 Exodus 25:1

Bwana akanena na Musa, akamwambia,

Kutoka 25:2 Exodus 25:2

Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu.

Kutoka 25:3 Exodus 25:3

Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii; dhahabu, na fedha, na shaba,

Kutoka 25:4 Exodus 25:4

na nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani safi, na singa za mbuzi;

Kutoka 25:5 Exodus 25:5

na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, na miti ya mshita,

Kutoka 25:6 Exodus 25:6

na mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri;

Kutoka 25:7 Exodus 25:7

na vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile naivera, na kwa kile kifuko cha kifuani.

Kutoka 25:8 Exodus 25:8

Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.

Kutoka 25:9 Exodus 25:9

Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya.

Kutoka 25:10 Exodus 25:10

Nao na wafanye sanduku la mti wa mshita; urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.

Kutoka 25:11 Exodus 25:11

Nawe ulifunike kwa dhahabu safi, ulifunike ndani na nje, nawe tia na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote.

Kutoka 25:12 Exodus 25:12

Nawe subu vikuku vinne vya dhahabu kwa ajili yake, na kuvitia katika miguu yake minne; vikuku viwili upande mmoja, na vikuku viwili upande wake wa pili.

Kutoka 25:13 Exodus 25:13

Nawe fanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu.

Kutoka 25:14 Exodus 25:14

Nawe tia hiyo miti katika vile vikuku vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku.

Kutoka 25:15 Exodus 25:15

Hiyo miti itakaa katika vile vikuku vya sanduku; haitaondolewa.

Kutoka 25:16 Exodus 25:16

Kisha tia ndani ya sanduku huo ushuhuda nitakaokupa.

Kutoka 25:17 Exodus 25:17

Nawe fanya kiti cha rehema cha dhahabu safi; urefu wake utakuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu.

Kutoka 25:18 Exodus 25:18

Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku.

Kutoka 25:19 Exodus 25:19

Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.

Kutoka 25:20 Exodus 25:20

Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema.

Kutoka 25:21 Exodus 25:21

Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku.

Kutoka 25:22 Exodus 25:22

Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.

Kutoka 25:23 Exodus 25:23

Nawe fanya meza ya mti wa mshita; urefu wake utakuwa dhiraa mbili, na upana wake dhiraa moja, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.

Kutoka 25:24 Exodus 25:24

Uifunike dhahabu safi, na kuifanyia ukingo wa dhahabu wa kuizunguka pande zote.

Kutoka 25:25 Exodus 25:25

Kisha ifanyie upapi wa kuizunguka pande zote, upana wake utakuwa nyanda nne, nawe uufanyie ule upapi ukingo wa urembo wa dhahabu wa kuuzunguka pande zote.

Kutoka 25:26 Exodus 25:26

Uifanyie vikuku vinne vya dhahabu, na kuvitia vile vikuku katika pembe zake nne, katika miguu yake minne.

Kutoka 25:27 Exodus 25:27

Vile vikuku na viwe karibu na ule upapi, ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza.

Kutoka 25:28 Exodus 25:28

Fanya ile miti ya mti wa mshita, na kuifunika dhahabu, kwamba ile meza ichukuliwe kwayo.

Kutoka 25:29 Exodus 25:29

Nawe fanya sahani zake, na miiko yake, na makopo yake, na vikombe vyake vya kumiminia; vifanye vyote vya dhahabu safi.

Kutoka 25:30 Exodus 25:30

Nawe utaiweka mikate ya wonyesho juu ya meza mbele yangu daima.

Kutoka 25:31 Exodus 25:31

Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, tako lake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho;

Kutoka 25:32 Exodus 25:32

nacho kitakuwa na matawi sita yenye kutoka ubavuni mwake; matawi matatu ya kinara upande wake mmoja, na matawi matatu ya kinara upande wake wa pili

Kutoka 25:33 Exodus 25:33

vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja; tovu na ua; na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua; vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara;

Kutoka 25:34 Exodus 25:34

na katika hicho kinara vikombe vinne vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake, na maua yake;

Kutoka 25:35 Exodus 25:35

na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, kwa hayo matawi sita yatokayo katika kile kinara.

Kutoka 25:36 Exodus 25:36

Matovu yake na matawi yake yatakuwa ya kitu kimoja nacho; kiwe chote pia kazi moja ya kufua, ya dhahabu safi.

Kutoka 25:37 Exodus 25:37

Nawe zifanye taa zake saba; nao wataziwasha hizo taa zake, zitoe nuru mbele yake.

Kutoka 25:38 Exodus 25:38

Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi.

Kutoka 25:39 Exodus 25:39

Kitafanywa cha talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo hivi vyote.

Kutoka 25:40 Exodus 25:40

Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, ulioonyeshwa mlimani.