Kutoka Mlango 17 Exodus

Kutoka 17:1 Exodus 17:1

Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama Bwana alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe.

Kutoka 17:2 Exodus 17:2

Kwa hiyo hao watu wakateta na Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwani kuteta na mimi? Mbona mnamjaribu Bwana?

Kutoka 17:3 Exodus 17:3

Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu?

Kutoka 17:4 Exodus 17:4

Musa akamlilia Bwana, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.

Kutoka 17:5 Exodus 17:5

Bwana akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe; na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaende.

Kutoka 17:6 Exodus 17:6

Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.

Kutoka 17:7 Exodus 17:7

Akapaita mahali pale jina lake Masa, na Meriba; kwa sababu ya mateto ya wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu Bwana, wakisema, Je! Bwana yu kati yetu au sivyo?

Kutoka 17:8 Exodus 17:8

Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.

Kutoka 17:9 Exodus 17:9

Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.

Kutoka 17:10 Exodus 17:10

Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima.

Kutoka 17:11 Exodus 17:11

Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.

Kutoka 17:12 Exodus 17:12

Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.

Kutoka 17:13 Exodus 17:13

Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga.

Kutoka 17:14 Exodus 17:14

Bwana akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.

Kutoka 17:15 Exodus 17:15

Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;

Kutoka 17:16 Exodus 17:16

akasema, Bwana ameapa; Bwana atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.