Marko Mlango 11 Mark

Marko 11:1 Mark 11:1

Hata walipokaribia Yerusalemu karibu na Bethfage na Bethania, kukabili mlima wa Mizeituni, aliwatuma wawili katika wanafunzi wake,

Marko 11:2 Mark 11:2

akawaambia, Nendeni mpaka kile kijiji kinachowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtaona mwana-punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni.

Marko 11:3 Mark 11:3

Na mtu akiwaambia, Mbona mnafanya hivi? Semeni, Bwana anamhitaji na mara atamrudisha tena hapa.

Marko 11:4 Mark 11:4

Wakaenda zao, wakamwona mwana-punda amefungwa penye mlango, nje katika njia kuu, wakamfungua.

Marko 11:5 Mark 11:5

Baadhi ya watu waliosimama huko wakawaambia, Mnafanya nini kumfungua mwana-punda?

Marko 11:6 Mark 11:6

Wakawaambia kama Yesu alivyowaagiza, nao wakawaruhusu.

Marko 11:7 Mark 11:7

Wakamletea Yesu yule mwana-punda, wakatandika mavazi yao juu yake; akaketi juu yake.

Marko 11:8 Mark 11:8

Watu wengi wakatandaza mavazi yao njiani, na wengine matawi waliyoyakata mashambani.

Marko 11:9 Mark 11:9

Nao watu waliotangulia na wale waliofuata wakapaza sauti, Hosana; ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana;

Marko 11:10 Mark 11:10

umebarikiwa na ufalme ujao, wa baba yetu Daudi. Hosana juu mbinguni.

Marko 11:11 Mark 11:11

Naye akaingia Yerusalemu hata ndani ya hekalu; na alipokwisha kutazama yote pande zote, kwa kuwa ni wakati wa jioni, akatoka, akaenda Bethania pamoja na wale Thenashara.

Marko 11:12 Mark 11:12

Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa.

Marko 11:13 Mark 11:13

Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.

Marko 11:14 Mark 11:14

Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia.

Marko 11:15 Mark 11:15

Wakafika Yerusalemu, naye akaingia ndani ya hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao wauzao njiwa;

Marko 11:16 Mark 11:16

wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya hekalu.

Marko 11:17 Mark 11:17

Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.

Marko 11:18 Mark 11:18

Wakuu wa makuhani na waandishi wakapata habari wakatafuta jinsi ya kumwangamiza; maana walimwogopa, kwa sababu mkutano wote walishangaa kwa mafundisho yake.

Marko 11:19 Mark 11:19

Na kulipokuwa jioni alitoka mjini.

Marko 11:20 Mark 11:20

Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani.

Marko 11:21 Mark 11:21

Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka.

Marko 11:22 Mark 11:22

Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu.

Marko 11:23 Mark 11:23

Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.

Marko 11:24 Mark 11:24

Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

Marko 11:25 Mark 11:25

Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.

Marko 11:26 Mark 11:26

Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]

Marko 11:27 Mark 11:27

Wakafika Yerusalemu tena; hata alipokuwa akitembea hekaluni, walimwendea wakuu wa makuhani, na waandishi, na wazee,

Marko 11:28 Mark 11:28

wakamwambia, Ni kwa mamlaka gani unatenda mambo haya? Naye ni nani aliyekupa mamlaka hii uyatende haya?

Marko 11:29 Mark 11:29

Yesu akawaambia, Nitawauliza neno moja, nanyi mnijibu, kisha nitawaambia ni kwa mamlaka gani nayatenda haya.

Marko 11:30 Mark 11:30

Ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Nijibuni.

Marko 11:31 Mark 11:31

Wakasemezana wao kwa wao, wakisema, Kama tukisema, Ulitoka mbinguni, atasema, Mbona, basi, hamkumwamini?

Marko 11:32 Mark 11:32

Ila tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, -- waliogopa watu; maana watu wote walimwona Yohana kuwa nabii halisi.

Marko 11:33 Mark 11:33

Wakamjibu Yesu, wakasema, Hatujui. Yesu akawaambia, Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani nayatenda haya.