Marko Mlango 12 Mark

Marko 12:1 Mark 12:1

Akaanza kusema nao kwa mifano; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akazungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.

Marko 12:2 Mark 12:2

Hata kwa wakati wake akatuma mtumwa kwa wale wakulima, ili apokee kwa wakulima katika matunda ya mizabibu.

Marko 12:3 Mark 12:3

Wakamtwaa, wakampiga, wakamtoa nje, hana kitu.

Marko 12:4 Mark 12:4

Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, na huyo wakamtia jeraha za kichwa, wakamfanyia jeuri.

Marko 12:5 Mark 12:5

Akamtuma mwingine, huyo wakamwua; na wengine wengi, hawa wakiwapiga na hawa wakiwaua.

Marko 12:6 Mark 12:6

Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu.

Marko 12:7 Mark 12:7

Lakini wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu.

Marko 12:8 Mark 12:8

Wakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu.

Marko 12:9 Mark 12:9

basi atafanyaje yule bwana wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.

Marko 12:10 Mark 12:10

Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.

Marko 12:11 Mark 12:11

Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?

Marko 12:12 Mark 12:12

Nao wakatafuta kumkamata, wakaogopa mkutano; maana walitambua ya kwamba ule mfano amewanenea wao. Wakamwacha wakaenda zao.

Marko 12:13 Mark 12:13

Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodi, ili wamnase kwa maneno.

Marko 12:14 Mark 12:14

Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo?

Marko 12:15 Mark 12:15

Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione.

Marko 12:16 Mark 12:16

Wakaileta. Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya Kaisari.

Marko 12:17 Mark 12:17

Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana.

Marko 12:18 Mark 12:18

Kisha Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza na kusema,

Marko 12:19 Mark 12:19

Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe akampatie ndugu yake mzao.

Marko 12:20 Mark 12:20

Basi kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao.

Marko 12:21 Mark 12:21

Wa pili naye akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzao. Na wa tatu kadhalika;

Marko 12:22 Mark 12:22

hata na wote saba, wasiache mzao. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.

Marko 12:23 Mark 12:23

Basi, katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye.

Marko 12:24 Mark 12:24

Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?

Marko 12:25 Mark 12:25

Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.

Marko 12:26 Mark 12:26

Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?

Marko 12:27 Mark 12:27

Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana.

Marko 12:28 Mark 12:28

Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?

Marko 12:29 Mark 12:29

Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;

Marko 12:30 Mark 12:30

nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.

Marko 12:31 Mark 12:31

Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

Marko 12:32 Mark 12:32

Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye;

Marko 12:33 Mark 12:33

na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia.

Marko 12:34 Mark 12:34

Naye Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, alimwambia, Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo.

Marko 12:35 Mark 12:35

Hata Yesu alipokuwa akifundisha katika hekalu, alijibu, akasema, Husemaje waandishi ya kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi?

Marko 12:36 Mark 12:36

Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.

Marko 12:37 Mark 12:37

Daudi mwenyewe asema ni Bwana; basi amekuwaje mwanawe? Na mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.

Marko 12:38 Mark 12:38

Akawaambia katika mafundisho yake, Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni,

Marko 12:39 Mark 12:39

na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele katika karamu;

Marko 12:40 Mark 12:40

ambao hula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu; hawa watapata hukumu iliyo kubwa.

Marko 12:41 Mark 12:41

Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.

Marko 12:42 Mark 12:42

Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.

Marko 12:43 Mark 12:43

Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;

Marko 12:44 Mark 12:44

maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.