Marko Mlango 15 Mark

Marko 15:1 Mark 15:1

Mara kulipokuwa asubuhi wakuu wa makuhani walifanya shauri pamoja na wazee na waandishi na baraza nzima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta mbele ya Pilato.

Marko 15:2 Mark 15:2

Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu, akamwambia, Wewe wasema.

Marko 15:3 Mark 15:3

Nao wakuu wa makuhani walikuwa wakimshitaki mambo mengi.

Marko 15:4 Mark 15:4

Pilato akamwuliza tena akisema, Hujibu neno? Tazama ni mambo mangapi wanayokushitaki!

Marko 15:5 Mark 15:5

Wala Yesu hakujibu neno tena, hata Pilato akastaajabu.

Marko 15:6 Mark 15:6

Basi wakati wa sikukuu huwafungulia mfungwa mmoja, wamwombaye.

Marko 15:7 Mark 15:7

Palikuwa na mtu aitwaye Baraba, amefungwa pamoja na watu waliofanya fitina, na kufanya uuaji katika fitina ile.

Marko 15:8 Mark 15:8

Makutano wakaja, wakaanza kuomba awafanyie kama vile alivyozoea.

Marko 15:9 Mark 15:9

Pilato akawajibu, akisema, Je! Mnataka niwafungulie mfalme wa Wayahudi?

Marko 15:10 Mark 15:10

Kwa maana alitambua ya kuwa wakuu wa makuhani wamemtoa kwa husuda.

Marko 15:11 Mark 15:11

Lakini wakuu wa makuhani wakawataharakisha makutano, kwamba afadhali awafungulie Baraba.

Marko 15:12 Mark 15:12

Pilato akajibu tena akawaambia, Basi nimtendeje huyu mnayemnena kuwa ni mfalme wa Wayahudi?

Marko 15:13 Mark 15:13

Wakapiga kelele tena, Msulibishe.

Marko 15:14 Mark 15:14

Pilato akawaambia, Kwani, ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, Msulibishe.

Marko 15:15 Mark 15:15

Pilato akipenda kuwaridhisha makutano, akawafungulia Baraba; akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, ili asulibiwe.

Marko 15:16 Mark 15:16

Nao askari wakamchukua ndani ya behewa, ndiyo Praitorio (yaani, nyumba ya uliwali), wakakusanya pamoja kikosi kizima.

Marko 15:17 Mark 15:17

Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani;

Marko 15:18 Mark 15:18

wakaanza kumsalimu, Salamu, Mfalme wa Wayahudi!

Marko 15:19 Mark 15:19

Wakampiga mwanzi wa kichwa, wakamtemea mate, wakapiga magoti, wakamsujudia.

Marko 15:20 Mark 15:20

Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua lile vazi la rangi ya zambarau, wakamvika mavazi yake mwenyewe; wakamchukua nje ili wamsulibishe.

Marko 15:21 Mark 15:21

Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashamba, Simoni Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake.

Marko 15:22 Mark 15:22

Wakamleta mpaka mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la kichwa.

Marko 15:23 Mark 15:23

Wakampa mvinyo iliyotiwa manemane, asiipokee.

Marko 15:24 Mark 15:24

Wakamsulibisha, wakagawa mavazi yake, wakayapigia kura kila mtu atwae nini.

Marko 15:25 Mark 15:25

Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha.

Marko 15:26 Mark 15:26

Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI.

Marko 15:27 Mark 15:27

Na pamoja naye walisulibisha wanyang'anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. [

Marko 15:28 Mark 15:28

Basi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na waasi.]

Marko 15:29 Mark 15:29

Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa, wakisema, Ahaa! Wewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga katika siku tatu,

Marko 15:30 Mark 15:30

jiponye nafsi yako, ushuke msalabani.

Marko 15:31 Mark 15:31

Kadhalika na wakuu wa makuhani wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, Aliponya wengine; hawezi kujiponya mwenyewe.

Marko 15:32 Mark 15:32

Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Hata wale waliosulibiwa pamoja naye wakamfyolea.

Marko 15:33 Mark 15:33

Na ilipokuwa saa sita, palikuwa na giza juu ya nchi yote, hata saa tisa.

Marko 15:34 Mark 15:34

Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

Marko 15:35 Mark 15:35

Na baadhi yao waliosimama pale, walisema, Tazama, anamwita Eliya.

Marko 15:36 Mark 15:36

Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha.

Marko 15:37 Mark 15:37

Naye Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.

Marko 15:38 Mark 15:38

Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini.

Marko 15:39 Mark 15:39

Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

Marko 15:40 Mark 15:40

Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;

Marko 15:41 Mark 15:41

hao ndio waliofuatana naye huko Galilaya, na kumtumikia; na wengine wengi waliopanda pamoja naye mpaka Yerusalemu.

Marko 15:42 Mark 15:42

Hata ikiisha kuwa jioni, kwa sababu ni Maandalio, ndiyo siku iliyo kabla ya sabato,

Marko 15:43 Mark 15:43

akaenda Yusufu, mtu wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza ya mashauri, naye mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu.

Marko 15:44 Mark 15:44

Lakini Pilato akastaajabu, kwamba amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo.

Marko 15:45 Mark 15:45

Hata alipokwisha kupata hakika kwa yule akida, alimpa Yusufu yule maiti.

Marko 15:46 Mark 15:46

Naye akanunua sanda ya kitani, akamtelemsha, akamfungia ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani; akavingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi.

Marko 15:47 Mark 15:47

Nao Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yose wakapatazama mahali alipowekwa.