Marko Mlango 9 Mark

Marko 9:1 Mark 9:1

Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.

Marko 9:2 Mark 9:2

Hata baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani, peke yao; akageuka sura yake mbele yao;

Marko 9:3 Mark 9:3

mavazi yake yakimeta-meta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe.

Marko 9:4 Mark 9:4

Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakizungumza na Yesu.

Marko 9:5 Mark 9:5

Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabi, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya.

Marko 9:6 Mark 9:6

Maana, hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na hofu nyingi.

Marko 9:7 Mark 9:7

Kisha likatokea wingu, likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.

Marko 9:8 Mark 9:8

Mara hiyo walipotazama huku na huku, hawakuona mtu pamoja nao ila Yesu peke yake.

Marko 9:9 Mark 9:9

Na walipokuwa wakishuka mlimani aliwakataza wasimweleze mtu waliyoyaona, hata Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu.

Marko 9:10 Mark 9:10

Wakalishika neno lile, wakiulizana wao kwa wao, Huko kufufuka katika wafu maana yake nini?

Marko 9:11 Mark 9:11

Wakamwuliza, wakisema, Mbona waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?

Marko 9:12 Mark 9:12

Akajibu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejeza upya yote; lakini, pamoja na haya, ameandikiwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharauliwa?

Marko 9:13 Mark 9:13

Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa.

Marko 9:14 Mark 9:14

Hata walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi wakijadiliana nao;

Marko 9:15 Mark 9:15

mara mkutano wote walipomwona walishangaa, wakamwendea mbio, wakamsalimu.

Marko 9:16 Mark 9:16

Akawauliza, Mnajadiliana nini nao?

Marko 9:17 Mark 9:17

Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu;

Marko 9:18 Mark 9:18

na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze.

Marko 9:19 Mark 9:19

Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu.

Marko 9:20 Mark 9:20

Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu.

Marko 9:21 Mark 9:21

Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto.

Marko 9:22 Mark 9:22

Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia.

Marko 9:23 Mark 9:23

Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.

Marko 9:24 Mark 9:24

Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.

Marko 9:25 Mark 9:25

Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.

Marko 9:26 Mark 9:26

Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa.

Marko 9:27 Mark 9:27

Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama.

Marko 9:28 Mark 9:28

Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?

Marko 9:29 Mark 9:29

Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.

Marko 9:30 Mark 9:30

Wakatoka huko, wakapita katikati ya Galilaya; naye hakutaka mtu kujua.

Marko 9:31 Mark 9:31

Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hata akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka.

Marko 9:32 Mark 9:32

Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza.

Marko 9:33 Mark 9:33

Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani?

Marko 9:34 Mark 9:34

Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa.

Marko 9:35 Mark 9:35

Akaketi chini, akawaita wale Thenashara akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote.

Marko 9:36 Mark 9:36

Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia,

Marko 9:37 Mark 9:37

Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.

Marko 9:38 Mark 9:38

Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi.

Marko 9:39 Mark 9:39

Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya;

Marko 9:40 Mark 9:40

kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.

Marko 9:41 Mark 9:41

Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.

Marko 9:42 Mark 9:42

Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini.

Marko 9:43 Mark 9:43

Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;

Marko 9:44 Mark 9:44

ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.
45

Marko 9:46 Mark 9:46

ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.

Marko 9:47 Mark 9:47

Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;

Marko 9:48 Mark 9:48

ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.

Marko 9:49 Mark 9:49

Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto.

Marko 9:50 Mark 9:50

Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.