Marko Mlango 6 Mark

Marko 6:1 Mark 6:1

Akatoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao; wanafunzi wake wakamfuata.

Marko 6:2 Mark 6:2

Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?

Marko 6:3 Mark 6:3

Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.

Marko 6:4 Mark 6:4

Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake.

Marko 6:5 Mark 6:5

Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya.

Marko 6:6 Mark 6:6

Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazunguka-zunguka katika vile vijiji, akifundisha.

Marko 6:7 Mark 6:7

Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;

Marko 6:8 Mark 6:8

akawakataza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa fimbo tu; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni;

Marko 6:9 Mark 6:9

lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili.

Marko 6:10 Mark 6:10

Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale.

Marko 6:11 Mark 6:11

Na mahali po pote wasipowakaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakung'uteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu, kuwa ushuhuda kwao.

Marko 6:12 Mark 6:12

Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu.

Marko 6:13 Mark 6:13

Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza.

Marko 6:14 Mark 6:14

Naye Mfalme Herode akasikia habari; kwa maana jina lake lilikuwa kutangaa, akasema, Yohana Mbatizaji amefufuka katika wafu, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake.

Marko 6:15 Mark 6:15

Wengine walisema, Ni Eliya. Wengine walisema, Huyu ni nabii, au ni kama mmoja wa manabii.

Marko 6:16 Mark 6:16

Lakini Herode aliposikia, alisema, Yohana, niliyemkata kichwa, amefufuka.

Marko 6:17 Mark 6:17

Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo ndugu yake, kwa kuwa amemwoa;

Marko 6:18 Mark 6:18

kwa sababu Yohana alimwambia Herode, Si halali kwako kuwa na mke wa nduguyo.

Marko 6:19 Mark 6:19

Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate.

Marko 6:20 Mark 6:20

Maana Herode alimwogopa Yohana; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha.

Marko 6:21 Mark 6:21

Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya;

Marko 6:22 Mark 6:22

ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lo lote utakalo, nitakupa.

Marko 6:23 Mark 6:23

Akamwapia, Lo lote utakaloniomba nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu.

Marko 6:24 Mark 6:24

Basi akatoka, akamwuliza mamaye, Niombe nini? Naye akasema, Kichwa cha Yohana Mbatizaji.

Marko 6:25 Mark 6:25

Mara akaingia kwa haraka mbele ya mfalme, akaomba akisema, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.

Marko 6:26 Mark 6:26

Mfalme akafanya huzuni sana, lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya hao walioketi karamuni, hakutaka kumkatalia.

Marko 6:27 Mark 6:27

Mara mfalme akatuma askari, akaamuru kuleta kichwa chake. Basi akaenda, akamkata kichwa mle gerezani,

Marko 6:28 Mark 6:28

akakileta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, naye yule kijana akampa mamaye.

Marko 6:29 Mark 6:29

Wanafunzi wake waliposikia habari, walikwenda, wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini.

Marko 6:30 Mark 6:30

Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa habari za mambo yote waliyoyafanya, na mambo yote waliyoyafundisha.

Marko 6:31 Mark 6:31

Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula.

Marko 6:32 Mark 6:32

Wakaenda zao faragha mashuani, mahali pasipokuwa na watu.

Marko 6:33 Mark 6:33

Watu wakawaona wakienda zao, na wengi wakatambua, wakaenda huko mbio kwa miguu, toka miji yote, wakatangulia kufika.

Marko 6:34 Mark 6:34

Naye aliposhuka mashuani, akaona mkutano mkuu, akawahurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi.

Marko 6:35 Mark 6:35

Hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa;

Marko 6:36 Mark 6:36

uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula.

Marko 6:37 Mark 6:37

Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakamwambia, Je! Twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili ili tuwape kula?

Marko 6:38 Mark 6:38

Akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakasema, Mitano, na samaki wawili.

Marko 6:39 Mark 6:39

Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabichi.

Marko 6:40 Mark 6:40

Wakaketi safu safu, hapa mia hapa hamsini.

Marko 6:41 Mark 6:41

Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; na wale samaki wawili akawagawia wote.

Marko 6:42 Mark 6:42

Wakala wote wakashiba.

Marko 6:43 Mark 6:43

Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki pia.

Marko 6:44 Mark 6:44

Na walioila ile mikate wapata elfu tano wanaume.

Marko 6:45 Mark 6:45

Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani, watangulie kwenda ng'ambo hata Bethsaida, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.

Marko 6:46 Mark 6:46

Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba.

Marko 6:47 Mark 6:47

Na kulipokuwa jioni mashua ilikuwa katikati ya bahari, na yeye yu peke yake katika nchi kavu.

Marko 6:48 Mark 6:48

Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita.

Marko 6:49 Mark 6:49

Nao walipomwona anatembea juu ya bahari, walidhani ya kuwa ni kivuli, wakapiga yowe,

Marko 6:50 Mark 6:50

kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope.

Marko 6:51 Mark 6:51

Akapanda mle chomboni walimo; upepo ukakoma; wakashangaa sana mioyoni mwao;

Marko 6:52 Mark 6:52

kwa maana hawakufahamu habari za ile mikate, lakini mioyo yao ilikuwa mizito.

Marko 6:53 Mark 6:53

Hata walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti, wakatia nanga.

Marko 6:54 Mark 6:54

Nao wakiisha kutoka mashuani, mara watu walimtambua,

Marko 6:55 Mark 6:55

wakaenda mbio, wakizunguka nchi ile yote, wakaanza kuwachukua vitandani walio hawawezi, kwenda kila mahali waliposikia kwamba yupo.

Marko 6:56 Mark 6:56

Na kila alikokwenda, akiingia vijijini, au mijini, au mashambani, wakawaweka wagonjwa sokoni, wakamsihi waguse ngaa pindo la vazi lake; nao wote waliomgusa wakapona.