Marko Mlango 13 Mark

Marko 13:1 Mark 13:1

Hata alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, Mwalimu, tazama, yalivyo mawe na majengo haya!

Marko 13:2 Mark 13:2

Yesu akajibu, akamwambia, Wayaona majengo haya makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.

Marko 13:3 Mark 13:3

Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, kuelekea hekalu Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea walimwuliza kwa faragha,

Marko 13:4 Mark 13:4

Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya wakati, hayo yote yatakapokuwa karibu kutimia?

Marko 13:5 Mark 13:5

Yesu akaanza kuwaambia, Jihadharini, mtu asiwadanganye.

Marko 13:6 Mark 13:6

Wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye, nao watadanganya wengi.

Marko 13:7 Mark 13:7

Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado.

Marko 13:8 Mark 13:8

Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na matetemeko ya nchi mahali mahali; kutakuwako na njaa; hayo ndiyo mwanzo wa utungu.

Marko 13:9 Mark 13:9

Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.

Marko 13:10 Mark 13:10

Na sharti Injili ihubiriwe kwanza katika mataifa yote.

Marko 13:11 Mark 13:11

Na watakapowachukua ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu.

Marko 13:12 Mark 13:12

Na ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, na baba atamsaliti mtoto, na watoto watashambulia wazazi wao, na kuwafisha.

Marko 13:13 Mark 13:13

Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

Marko 13:14 Mark 13:14

Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani;

Marko 13:15 Mark 13:15

na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake;

Marko 13:16 Mark 13:16

naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake.

Marko 13:17 Mark 13:17

Lakini ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku hizo!

Marko 13:18 Mark 13:18

Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi.

Marko 13:19 Mark 13:19

Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe.

Marko 13:20 Mark 13:20

Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo.

Marko 13:21 Mark 13:21

Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki;

Marko 13:22 Mark 13:22

kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule.

Marko 13:23 Mark 13:23

Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele.

Marko 13:24 Mark 13:24

Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake.

Marko 13:25 Mark 13:25

na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika.

Marko 13:26 Mark 13:26

Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu.

Marko 13:27 Mark 13:27

Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu.

Marko 13:28 Mark 13:28

Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu;

Marko 13:29 Mark 13:29

nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni.

Marko 13:30 Mark 13:30

Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie.

Marko 13:31 Mark 13:31

Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Marko 13:32 Mark 13:32

Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.

Marko 13:33 Mark 13:33

Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.

Marko 13:34 Mark 13:34

Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.

Marko 13:35 Mark 13:35

Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi;

Marko 13:36 Mark 13:36

asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.

Marko 13:37 Mark 13:37

Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.