Marko Mlango 7 Mark

Marko 7:1 Mark 7:1

Kisha Mafarisayo, na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemu, wakakusanyika mbele yake,

Marko 7:2 Mark 7:2

wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa.

Marko 7:3 Mark 7:3

Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao;

Marko 7:4 Mark 7:4

tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.

Marko 7:5 Mark 7:5

Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi?

Marko 7:6 Mark 7:6

Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami;

Marko 7:7 Mark 7:7

Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu,

Marko 7:8 Mark 7:8

Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.

Marko 7:9 Mark 7:9

Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.

Marko 7:10 Mark 7:10

Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe.

Marko 7:11 Mark 7:11

Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi;

Marko 7:12 Mark 7:12

wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye;

Marko 7:13 Mark 7:13

huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.

Marko 7:14 Mark 7:14

Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu.

Marko 7:15 Mark 7:15

Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu.

Marko 7:16 Mark 7:16

Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.]

Marko 7:17 Mark 7:17

Hata alipoingia nyumbani, ameuacha mkutano, wanafunzi wake wakamwuliza habari za ule mfano.

Marko 7:18 Mark 7:18

Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;

Marko 7:19 Mark 7:19

kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.

Marko 7:20 Mark 7:20

Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.

Marko 7:21 Mark 7:21

Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

Marko 7:22 Mark 7:22

wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

Marko 7:23 Mark 7:23

Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.

Marko 7:24 Mark 7:24

Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika.

Marko 7:25 Mark 7:25

Ila mara mwanamke, ambaye binti yake yuna pepo mchafu, alisikia habari zake, akaja akamwangukia miguuni pake.

Marko 7:26 Mark 7:26

Na yule mwanamke ni Myunani, kabila yake ni Msirofoinike. Akamwomba amtoe pepo katika binti yake.

Marko 7:27 Mark 7:27

Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa.

Marko 7:28 Mark 7:28

Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.

Marko 7:29 Mark 7:29

Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, enenda zako, pepo amemtoka binti yako.

Marko 7:30 Mark 7:30

Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka.

Marko 7:31 Mark 7:31

Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli.

Marko 7:32 Mark 7:32

Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono.

Marko 7:33 Mark 7:33

Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi,

Marko 7:34 Mark 7:34

akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka.

Marko 7:35 Mark 7:35

Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.

Marko 7:36 Mark 7:36

Akawaonya wasimwambie mtu; lakini kadiri ya alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari;

Marko 7:37 Mark 7:37

wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme.