Marko Mlango 16 Mark

Marko 16:1 Mark 16:1

Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka.

Marko 16:2 Mark 16:2

Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;

Marko 16:3 Mark 16:3

wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi?

Marko 16:4 Mark 16:4

Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno.

Marko 16:5 Mark 16:5

Wakaingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu.

Marko 16:6 Mark 16:6

Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka.

Marko 16:7 Mark 16:7

Lakini enendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya; huko mtamwona, kama alivyowaambia.

Marko 16:8 Mark 16:8

Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingia tetemeko na ushangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa. [

Marko 16:9 Mark 16:9

Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.

Marko 16:10 Mark 16:10

Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia.

Marko 16:11 Mark 16:11

Walakini hao waliposikia kama yu hai, naye amemwona, hawakusadiki.

Marko 16:12 Mark 16:12

Baada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba.

Marko 16:13 Mark 16:13

Na hao wakaenda zao wakawapa habari wale wengine; wala hao hawakuwasadiki.

Marko 16:14 Mark 16:14

Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu.

Marko 16:15 Mark 16:15

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Marko 16:16 Mark 16:16

Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

Marko 16:17 Mark 16:17

Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;

Marko 16:18 Mark 16:18

watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Marko 16:19 Mark 16:19

Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.

Marko 16:20 Mark 16:20

Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]