Marko Mlango 3 Mark

Marko 3:1 Mark 3:1

Akaingia tena katika sinagogi; na palikuwako huko mtu mwenye mkono uliopooza;

Marko 3:2 Mark 3:2

wakamvizia ili kuona kama atamponya siku ya sabato; wapate kumshitaki.

Marko 3:3 Mark 3:3

Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, Simama katikati.

Marko 3:4 Mark 3:4

Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.

Marko 3:5 Mark 3:5

Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.

Marko 3:6 Mark 3:6

Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza.

Marko 3:7 Mark 3:7

Naye Yesu akajitenga, yeye na wanafunzi wake, akaenda baharini. Mkutano mkuu ukamfuata, kutoka Galilaya, na Uyahudi,

Marko 3:8 Mark 3:8

na Yerusalemu, na Idumaya, na ng'ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea.

Marko 3:9 Mark 3:9

Akawaambia wanafunzi wake ya kwamba chombo kidogo kikae karibu naye, kwa sababu ya mkutano, wasije wakamsonga.

Marko 3:10 Mark 3:10

Maana aliponya wengi, hata wote waliokuwa na misiba wakamrukia wapate kumgusa.

Marko 3:11 Mark 3:11

Na pepo wachafu, kila walipomwona, walianguka mbele yake, wakalia wakisema, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.

Marko 3:12 Mark 3:12

Akawakataza sana, wasimdhihirishe.

Marko 3:13 Mark 3:13

Akapanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea.

Marko 3:14 Mark 3:14

Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri,

Marko 3:15 Mark 3:15

tena wawe na amri ya kutoa pepo.

Marko 3:16 Mark 3:16

Akawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina la Petro;

Marko 3:17 Mark 3:17

na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo;

Marko 3:18 Mark 3:18

na Andrea, na Filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thadayo, na Simoni Mkananayo,

Marko 3:19 Mark 3:19

na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti. Kisha akaingia nyumbani.

Marko 3:20 Mark 3:20

Mkutano wakakusanyika tena, hata wao wenyewe wasiweze hata kula mkate.

Marko 3:21 Mark 3:21

Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.

Marko 3:22 Mark 3:22

Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo.

Marko 3:23 Mark 3:23

Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani?

Marko 3:24 Mark 3:24

Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama;

Marko 3:25 Mark 3:25

na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.

Marko 3:26 Mark 3:26

Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo.

Marko 3:27 Mark 3:27

Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.

Marko 3:28 Mark 3:28

Amin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;

Marko 3:29 Mark 3:29

bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,

Marko 3:30 Mark 3:30

kwa vile walivyosema, Ana pepo mchafu.

Marko 3:31 Mark 3:31

Wakaja mamaye na nduguze; wakasimama nje, wakatuma mtu kumwita.

Marko 3:32 Mark 3:32

Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka, wakamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.

Marko 3:33 Mark 3:33

Akawajibu, akisema, Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?

Marko 3:34 Mark 3:34

Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu!

Marko 3:35 Mark 3:35

Kwa maana mtu ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.