Marko Mlango 5 Mark

Marko 5:1 Mark 5:1

Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi.

Marko 5:2 Mark 5:2

Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;

Marko 5:3 Mark 5:3

makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;

Marko 5:4 Mark 5:4

kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda.

Marko 5:5 Mark 5:5

Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe.

Marko 5:6 Mark 5:6

Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia;

Marko 5:7 Mark 5:7

akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.

Marko 5:8 Mark 5:8

Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu.

Marko 5:9 Mark 5:9

Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.

Marko 5:10 Mark 5:10

Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile.

Marko 5:11 Mark 5:11

Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha.

Marko 5:12 Mark 5:12

Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.

Marko 5:13 Mark 5:13

Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.

Marko 5:14 Mark 5:14

Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.

Marko 5:15 Mark 5:15

Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa.

Marko 5:16 Mark 5:16

Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe.

Marko 5:17 Mark 5:17

Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao.

Marko 5:18 Mark 5:18

Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye;

Marko 5:19 Mark 5:19

lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu.

Marko 5:20 Mark 5:20

Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.

Marko 5:21 Mark 5:21

Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.

Marko 5:22 Mark 5:22

Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake,

Marko 5:23 Mark 5:23

akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.

Marko 5:24 Mark 5:24

Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa.

Marko 5:25 Mark 5:25

Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili,

Marko 5:26 Mark 5:26

na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya

Marko 5:27 Mark 5:27

aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;

Marko 5:28 Mark 5:28

maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.

Marko 5:29 Mark 5:29

Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.

Marko 5:30 Mark 5:30

Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu?

Marko 5:31 Mark 5:31

Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusonga-songa, nawe wasema, Ni nani aliyenigusa?

Marko 5:32 Mark 5:32

Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo.

Marko 5:33 Mark 5:33

Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote.

Marko 5:34 Mark 5:34

Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.

Marko 5:35 Mark 5:35

Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu?

Marko 5:36 Mark 5:36

Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu.

Marko 5:37 Mark 5:37

Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye Yakobo.

Marko 5:38 Mark 5:38

Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu.

Marko 5:39 Mark 5:39

Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu.

Marko 5:40 Mark 5:40

Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana.

Marko 5:41 Mark 5:41

Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka.

Marko 5:42 Mark 5:42

Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu.

Marko 5:43 Mark 5:43

Akawaonya sana, mtu asijue habari ile; akaamuru apewe chakula.