Yohana Mlango 13 John

Yohana 13:1 John 13:1

Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo.

Yohana 13:2 John 13:2

Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti;

Yohana 13:3 John 13:3

Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,

Yohana 13:4 John 13:4

aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni.

Yohana 13:5 John 13:5

Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.

Yohana 13:6 John 13:6

Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?

Yohana 13:7 John 13:7

Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.

Yohana 13:8 John 13:8

Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.

Yohana 13:9 John 13:9

Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia.

Yohana 13:10 John 13:10

Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.

Yohana 13:11 John 13:11

Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi.

Yohana 13:12 John 13:12

Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea?

Yohana 13:13 John 13:13

Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.

Yohana 13:14 John 13:14

Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.

Yohana 13:15 John 13:15

Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.

Yohana 13:16 John 13:16

Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.

Yohana 13:17 John 13:17

Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.

Yohana 13:18 John 13:18

Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake.

Yohana 13:19 John 13:19

Tangu sasa nawaambia kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye.

Yohana 13:20 John 13:20

Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu ye yote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenipeleka.

Yohana 13:21 John 13:21

Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.

Yohana 13:22 John 13:22

Wanafunzi wakatazamana, huku wakiona shaka ni nani amtajaye.

Yohana 13:23 John 13:23

Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda.

Yohana 13:24 John 13:24

Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye?

Yohana 13:25 John 13:25

Basi yeye, hali akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?

Yohana 13:26 John 13:26

Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote.

Yohana 13:27 John 13:27

Na baada ya hilo tonge Shetani alimwingia. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi.

Yohana 13:28 John 13:28

Wala hakuna mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu ya kumwambia hivyo.

Yohana 13:29 John 13:29

Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu.

Yohana 13:30 John 13:30

Basi huyo, akiisha kulipokea lile tonge, akatoka mara hiyo. Nako kulikuwa ni usiku.

Yohana 13:31 John 13:31

Basi huyo alipokwisha kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye Mungu ametukuzwa ndani yake.

Yohana 13:32 John 13:32

Mungu naye atamtukuza ndani ya nafsi yake; naye atamtukuza mara.

Yohana 13:33 John 13:33

Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.

Yohana 13:34 John 13:34

Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.

Yohana 13:35 John 13:35

Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.

Yohana 13:36 John 13:36

Simoni Petro akamwambia, Bwana, unakwendapi? Yesu akamjibu, Niendako huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadaye.

Yohana 13:37 John 13:37

Petro akamwambia, Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako.

Yohana 13:38 John 13:38

Yesu akamjibu, Je! Wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jimbi hatawika hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu.