Yohana Mlango 15 John

Yohana 15:1 John 15:1

Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.

Yohana 15:2 John 15:2

Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.

Yohana 15:3 John 15:3

Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.

Yohana 15:4 John 15:4

Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.

Yohana 15:5 John 15:5

Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.

Yohana 15:6 John 15:6

Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.

Yohana 15:7 John 15:7

Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

Yohana 15:8 John 15:8

Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.

Yohana 15:9 John 15:9

Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu.

Yohana 15:10 John 15:10

Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

Yohana 15:11 John 15:11

Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.

Yohana 15:12 John 15:12

Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.

Yohana 15:13 John 15:13

Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

Yohana 15:14 John 15:14

Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.

Yohana 15:15 John 15:15

Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.

Yohana 15:16 John 15:16

Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

Yohana 15:17 John 15:17

Haya nawaamuru ninyi, mpate kupendana.

Yohana 15:18 John 15:18

Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.

Yohana 15:19 John 15:19

Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.

Yohana 15:20 John 15:20

Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.

Yohana 15:21 John 15:21

Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka.

Yohana 15:22 John 15:22

Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.

Yohana 15:23 John 15:23

Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu.

Yohana 15:24 John 15:24

Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.

Yohana 15:25 John 15:25

Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure.

Yohana 15:26 John 15:26

Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.

Yohana 15:27 John 15:27

Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami.