Yohana Mlango 7 John

Yohana 7:1 John 7:1

Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua.

Yohana 7:2 John 7:2

Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.

Yohana 7:3 John 7:3

Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya.

Yohana 7:4 John 7:4

Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu.

Yohana 7:5 John 7:5

Maana hata nduguze hawakumwamini.

Yohana 7:6 John 7:6

Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo.

Yohana 7:7 John 7:7

Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.

Yohana 7:8 John 7:8

Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu.

Yohana 7:9 John 7:9

Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya.

Yohana 7:10 John 7:10

Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.

Yohana 7:11 John 7:11

Basi Wayahudi wakamtafuta kwenye sikukuu, wakasema, Yuko wapi yule?

Yohana 7:12 John 7:12

Kukawa na manung'uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano.

Yohana 7:13 John 7:13

Walakini hakuna mtu aliyemtaja waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.

Yohana 7:14 John 7:14

Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alikwea kuingia hekaluni, akafundisha.

Yohana 7:15 John 7:15

Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma?

Yohana 7:16 John 7:16

Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka.

Yohana 7:17 John 7:17

Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.

Yohana 7:18 John 7:18

Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu.

Yohana 7:19 John 7:19

Je! Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua?

Yohana 7:20 John 7:20

Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua?

Yohana 7:21 John 7:21

Yesu akajibu, akawaambia, Mimi nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnaistaajabia.

Yohana 7:22 John 7:22

Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi siku ya sabato humtahiri mtu.

Yohana 7:23 John 7:23

Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?

Yohana 7:24 John 7:24

Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.

Yohana 7:25 John 7:25

Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue?

Yohana 7:26 John 7:26

Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo?

Yohana 7:27 John 7:27

Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako.

Yohana 7:28 John 7:28

Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi.

Yohana 7:29 John 7:29

Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.

Yohana 7:30 John 7:30

Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.

Yohana 7:31 John 7:31

Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?

Yohana 7:32 John 7:32

Mafarisayo wakawasikia mkutano wakinung'unika hivi juu yake; basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma watumishi ili wamkamate.

Yohana 7:33 John 7:33

Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka.

Yohana 7:34 John 7:34

Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja.

Yohana 7:35 John 7:35

Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa Utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani?

Yohana 7:36 John 7:36

Ni neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja?

Yohana 7:37 John 7:37

Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.

Yohana 7:38 John 7:38

Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

Yohana 7:39 John 7:39

Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.

Yohana 7:40 John 7:40

Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.

Yohana 7:41 John 7:41

Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya?

Yohana 7:42 John 7:42

Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?

Yohana 7:43 John 7:43

Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake.

Yohana 7:44 John 7:44

Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika.

Yohana 7:45 John 7:45

Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta?

Yohana 7:46 John 7:46

Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena.

Yohana 7:47 John 7:47

Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika?

Yohana 7:48 John 7:48

Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?

Yohana 7:49 John 7:49

Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa.

Yohana 7:50 John 7:50

Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao),

Yohana 7:51 John 7:51

Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo?

Yohana 7:52 John 7:52

Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya!

Yohana 7:53 John 7:53

Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.