Yohana Mlango 12 John

Yohana 12:1 John 12:1

Basi, siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu.

Yohana 12:2 John 12:2

Basi wakamwandalia karamu huko; naye Martha akatumikia; na Lazaro alikuwa mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye.

Yohana 12:3 John 12:3

Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.

Yohana 12:4 John 12:4

Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema,

Yohana 12:5 John 12:5

Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini?

Yohana 12:6 John 12:6

Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.

Yohana 12:7 John 12:7

Basi Yesu alisema, Mwache aiweke kwa siku ya maziko yangu.

Yohana 12:8 John 12:8

Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamnami sikuzote.

Yohana 12:9 John 12:9

Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu.

Yohana 12:10 John 12:10

Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye;

Yohana 12:11 John 12:11

maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walijitenga, wakamwamini Yesu.

Yohana 12:12 John 12:12

Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu;

Yohana 12:13 John 12:13

wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!

Yohana 12:14 John 12:14

Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa,

Yohana 12:15 John 12:15

Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda.

Yohana 12:16 John 12:16

Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo.

Yohana 12:17 John 12:17

Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua.

Yohana 12:18 John 12:18

Na kwa sababu hiyo mkutano walikwenda kumlaki, kwa kuwa wamesikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo.

Yohana 12:19 John 12:19

Basi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno lo lote; tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.

Yohana 12:20 John 12:20

Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu.

Yohana 12:21 John 12:21

Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu.

Yohana 12:22 John 12:22

Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu.

Yohana 12:23 John 12:23

Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu.

Yohana 12:24 John 12:24

Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.

Yohana 12:25 John 12:25

Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.

Yohana 12:26 John 12:26

Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.

Yohana 12:27 John 12:27

Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.

Yohana 12:28 John 12:28

Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.

Yohana 12:29 John 12:29

Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye.

Yohana 12:30 John 12:30

Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu.

Yohana 12:31 John 12:31

Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.

Yohana 12:32 John 12:32

Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.

Yohana 12:33 John 12:33

Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa.

Yohana 12:34 John 12:34

Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?

Yohana 12:35 John 12:35

Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.

Yohana 12:36 John 12:36

Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha wasimwone.

Yohana 12:37 John 12:37

Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini;

Yohana 12:38 John 12:38

ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu; Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?

Yohana 12:39 John 12:39

Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema tena,

Yohana 12:40 John 12:40

Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

Yohana 12:41 John 12:41

Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa aliuona utukufu wake, akataja habari zake.

Yohana 12:42 John 12:42

Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi.

Yohana 12:43 John 12:43

Kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu.

Yohana 12:44 John 12:44

Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka.

Yohana 12:45 John 12:45

Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka.

Yohana 12:46 John 12:46

Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.

Yohana 12:47 John 12:47

Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.

Yohana 12:48 John 12:48

Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

Yohana 12:49 John 12:49

Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.

Yohana 12:50 John 12:50

Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.