Yohana Mlango 11 John

Yohana 11:1 John 11:1

Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.

Yohana 11:2 John 11:2

Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi.

Yohana 11:3 John 11:3

Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi.

Yohana 11:4 John 11:4

Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.

Yohana 11:5 John 11:5

Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro.

Yohana 11:6 John 11:6

Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo.

Yohana 11:7 John 11:7

Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena.

Yohana 11:8 John 11:8

Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?

Yohana 11:9 John 11:9

Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

Yohana 11:10 John 11:10

Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake.

Yohana 11:11 John 11:11

Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.

Yohana 11:12 John 11:12

Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona.

Yohana 11:13 John 11:13

Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi.

Yohana 11:14 John 11:14

Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa.

Yohana 11:15 John 11:15

Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake.

Yohana 11:16 John 11:16

Basi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi, ili tufe pamoja naye.

Yohana 11:17 John 11:17

Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne.

Yohana 11:18 John 11:18

Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi;

Yohana 11:19 John 11:19

na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao.

Yohana 11:20 John 11:20

Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani.

Yohana 11:21 John 11:21

Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.

Yohana 11:22 John 11:22

Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa.

Yohana 11:23 John 11:23

Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka.

Yohana 11:24 John 11:24

Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.

Yohana 11:25 John 11:25

Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;

Yohana 11:26 John 11:26

naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?

Yohana 11:27 John 11:27

Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.

Yohana 11:28 John 11:28

Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita.

Yohana 11:29 John 11:29

Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea.

Yohana 11:30 John 11:30

Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo pale pale alipomlaki Martha.

Yohana 11:31 John 11:31

Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko.

Yohana 11:32 John 11:32

Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.

Yohana 11:33 John 11:33

Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,

Yohana 11:34 John 11:34

akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame.

Yohana 11:35 John 11:35

Yesu akalia machozi.

Yohana 11:36 John 11:36

Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda.

Yohana 11:37 John 11:37

Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?

Yohana 11:38 John 11:38

Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.

Yohana 11:39 John 11:39

Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.

Yohana 11:40 John 11:40

Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?

Yohana 11:41 John 11:41

Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.

Yohana 11:42 John 11:42

Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.

Yohana 11:43 John 11:43

Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.

Yohana 11:44 John 11:44

Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.

Yohana 11:45 John 11:45

Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini.

Yohana 11:46 John 11:46

Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu.

Yohana 11:47 John 11:47

Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi.

Yohana 11:48 John 11:48

Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu.

Yohana 11:49 John 11:49

Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote;

Yohana 11:50 John 11:50

wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima.

Yohana 11:51 John 11:51

Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo.

Yohana 11:52 John 11:52

Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja.

Yohana 11:53 John 11:53

Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua.

Yohana 11:54 John 11:54

Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.

Yohana 11:55 John 11:55

Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; na wengi wakakwea toka mashambani kwenda Yerusalemu kabla ya Pasaka, ili wajitakase.

Yohana 11:56 John 11:56

Basi wao wakamtafuta Yesu, wakasemezana hali wamesimama hekaluni, Mwaonaje? Haji kabisa sikukuu hii?

Yohana 11:57 John 11:57

Na wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri ya kwamba mtu akimjua alipo, alete habari, ili wapate kumkamata.