Yohana Mlango 17 John

Yohana 17:1 John 17:1

Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe;

Yohana 17:2 John 17:2

kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.

Yohana 17:3 John 17:3

Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Yohana 17:4 John 17:4

Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

Yohana 17:5 John 17:5

Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

Yohana 17:6 John 17:6

Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.

Yohana 17:7 John 17:7

Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako.

Yohana 17:8 John 17:8

Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

Yohana 17:9 John 17:9

Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako;

Yohana 17:10 John 17:10

na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.

Yohana 17:11 John 17:11

Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

Yohana 17:12 John 17:12

Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

Yohana 17:13 John 17:13

Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

Yohana 17:14 John 17:14

Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

Yohana 17:15 John 17:15

Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.

Yohana 17:16 John 17:16

Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

Yohana 17:17 John 17:17

Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.

Yohana 17:18 John 17:18

Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.

Yohana 17:19 John 17:19

Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.

Yohana 17:20 John 17:20

Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.

Yohana 17:21 John 17:21

Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

Yohana 17:22 John 17:22

Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.

Yohana 17:23 John 17:23

Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.

Yohana 17:24 John 17:24

Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.

Yohana 17:25 John 17:25

Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.

Yohana 17:26 John 17:26

Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.