Yohana Mlango 2 John

Yohana 2:1 John 2:1

Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.

Yohana 2:2 John 2:2

Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.

Yohana 2:3 John 2:3

Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.

Yohana 2:4 John 2:4

Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.

Yohana 2:5 John 2:5

Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni.

Yohana 2:6 John 2:6

Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.

Yohana 2:7 John 2:7

Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.

Yohana 2:8 John 2:8

Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.

Yohana 2:9 John 2:9

Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,

Yohana 2:10 John 2:10

akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.

Yohana 2:11 John 2:11

Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

Yohana 2:12 John 2:12

Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko siku si nyingi.

Yohana 2:13 John 2:13

Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.

Yohana 2:14 John 2:14

Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.

Yohana 2:15 John 2:15

Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;

Yohana 2:16 John 2:16

akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.

Yohana 2:17 John 2:17

Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.

Yohana 2:18 John 2:18

Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya?

Yohana 2:19 John 2:19

Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.

Yohana 2:20 John 2:20

Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?

Yohana 2:21 John 2:21

Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.

Yohana 2:22 John 2:22

Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.

Yohana 2:23 John 2:23

Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya.

Yohana 2:24 John 2:24

Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote;

Yohana 2:25 John 2:25

na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.