Yohana Mlango 1 John

Yohana 1:1 John 1:1

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Yohana 1:2 John 1:2

Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

Yohana 1:3 John 1:3

Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

Yohana 1:4 John 1:4

Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

Yohana 1:5 John 1:5

Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.

Yohana 1:6 John 1:6

Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.

Yohana 1:7 John 1:7

Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.

Yohana 1:8 John 1:8

Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.

Yohana 1:9 John 1:9

Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.

Yohana 1:10 John 1:10

Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.

Yohana 1:11 John 1:11

Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.

Yohana 1:12 John 1:12

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

Yohana 1:13 John 1:13

waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Yohana 1:14 John 1:14

Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Yohana 1:15 John 1:15

Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.

Yohana 1:16 John 1:16

Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.

Yohana 1:17 John 1:17

Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.

Yohana 1:18 John 1:18

Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

Yohana 1:19 John 1:19

Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?

Yohana 1:20 John 1:20

Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo.

Yohana 1:21 John 1:21

Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.

Yohana 1:22 John 1:22

Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako?

Yohana 1:23 John 1:23

Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.

Yohana 1:24 John 1:24

Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo.

Yohana 1:25 John 1:25

Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?

Yohana 1:26 John 1:26

Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi.

Yohana 1:27 John 1:27

Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.

Yohana 1:28 John 1:28

Hayo yalifanyika huko Bethania ng'ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.

Yohana 1:29 John 1:29

Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!

Yohana 1:30 John 1:30

Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.

Yohana 1:31 John 1:31

Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji.

Yohana 1:32 John 1:32

Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake.

Yohana 1:33 John 1:33

Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.

Yohana 1:34 John 1:34

Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.

Yohana 1:35 John 1:35

Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake.

Yohana 1:36 John 1:36

Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!

Yohana 1:37 John 1:37

Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.

Yohana 1:38 John 1:38

Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi?

Yohana 1:39 John 1:39

Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.

Yohana 1:40 John 1:40

Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.

Yohana 1:41 John 1:41

Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).

Yohana 1:42 John 1:42

Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).

Yohana 1:43 John 1:43

Siku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate.

Yohana 1:44 John 1:44

Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro.

Yohana 1:45 John 1:45

Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.

Yohana 1:46 John 1:46

Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone.

Yohana 1:47 John 1:47

Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.

Yohana 1:48 John 1:48

Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona.

Yohana 1:49 John 1:49

Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli.

Yohana 1:50 John 1:50

Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya.

Yohana 1:51 John 1:51

Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.