Yohana Mlango 14 John

Yohana 14:1 John 14:1

Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

Yohana 14:2 John 14:2

Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

Yohana 14:3 John 14:3

Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

Yohana 14:4 John 14:4

Nami niendako mwaijua njia.

Yohana 14:5 John 14:5

Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?

Yohana 14:6 John 14:6

Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Yohana 14:7 John 14:7

Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.

Yohana 14:8 John 14:8

Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.

Yohana 14:9 John 14:9

Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?

Yohana 14:10 John 14:10

Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

Yohana 14:11 John 14:11

Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.

Yohana 14:12 John 14:12

Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

Yohana 14:13 John 14:13

Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.

Yohana 14:14 John 14:14

Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

Yohana 14:15 John 14:15

Mkinipenda, mtazishika amri zangu.

Yohana 14:16 John 14:16

Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

Yohana 14:17 John 14:17

ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

Yohana 14:18 John 14:18

Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

Yohana 14:19 John 14:19

Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.

Yohana 14:20 John 14:20

Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.

Yohana 14:21 John 14:21

Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.

Yohana 14:22 John 14:22

Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu?

Yohana 14:23 John 14:23

Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.

Yohana 14:24 John 14:24

Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.

Yohana 14:25 John 14:25

Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu.

Yohana 14:26 John 14:26

Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Yohana 14:27 John 14:27

Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.

Yohana 14:28 John 14:28

Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.

Yohana 14:29 John 14:29

Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini.

Yohana 14:30 John 14:30

Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.

Yohana 14:31 John 14:31

Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.