Luka Mlango 10 Luke

Luka 10:1 Luke 10:1

Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.

Luka 10:2 Luke 10:2

Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.

Luka 10:3 Luke 10:3

Enendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu.

Luka 10:4 Luke 10:4

Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani.

Luka 10:5 Luke 10:5

Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu;

Luka 10:6 Luke 10:6

na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu.

Luka 10:7 Luke 10:7

Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.

Luka 10:8 Luke 10:8

Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu;

Luka 10:9 Luke 10:9

waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.

Luka 10:10 Luke 10:10

Na mji wo wote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni,

Luka 10:11 Luke 10:11

Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung'uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.

Luka 10:12 Luke 10:12

Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo.

Luka 10:13 Luke 10:13

Ole wako Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu.

Luka 10:14 Luke 10:14

Lakini, siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko ninyi.

Luka 10:15 Luke 10:15

Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.

Luka 10:16 Luke 10:16

Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.

Luka 10:17 Luke 10:17

Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.

Luka 10:18 Luke 10:18

Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.

Luka 10:19 Luke 10:19

Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.

Luka 10:20 Luke 10:20

Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.

Luka 10:21 Luke 10:21

Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza.

Luka 10:22 Luke 10:22

Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.

Luka 10:23 Luke 10:23

Akawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi.

Luka 10:24 Luke 10:24

Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.

Luka 10:25 Luke 10:25

Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?

Luka 10:26 Luke 10:26

Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

Luka 10:27 Luke 10:27

Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

Luka 10:28 Luke 10:28

Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.

Luka 10:29 Luke 10:29

Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?

Luka 10:30 Luke 10:30

Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang'anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.

Luka 10:31 Luke 10:31

Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.

Luka 10:32 Luke 10:32

Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.

Luka 10:33 Luke 10:33

Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,

Luka 10:34 Luke 10:34

akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.

Luka 10:35 Luke 10:35

Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.

Luka 10:36 Luke 10:36

Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang'anyi?

Luka 10:37 Luke 10:37

Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.

Luka 10:38 Luke 10:38

Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake.

Luka 10:39 Luke 10:39

Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.

Luka 10:40 Luke 10:40

Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie.

Luka 10:41 Luke 10:41

Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi;

Luka 10:42 Luke 10:42

lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.