Luka Mlango 8 Luke

Luka 8:1 Luke 8:1

Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,

Luka 8:2 Luke 8:2

na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,

Luka 8:3 Luke 8:3

na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.

Luka 8:4 Luke 8:4

Mkutano mkuu ulipokutanika, na wale waliotoka kila mji wakimjia, alisema kwa mfano;

Luka 8:5 Luke 8:5

Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila.

Luka 8:6 Luke 8:6

Nyingine zikaanguka penye mwamba; zilipoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba.

Luka 8:7 Luke 8:7

Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga.

Luka 8:8 Luke 8:8

Nyingine zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja kwa mia. Alipokuwa akinena hayo alipaza sauti akisema, Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.

Luka 8:9 Luke 8:9

Wanafunzi wake wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo?

Luka 8:10 Luke 8:10

Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.

Luka 8:11 Luke 8:11

Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu.

Luka 8:12 Luke 8:12

Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.

Luka 8:13 Luke 8:13

Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.

Luka 8:14 Luke 8:14

Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote.

Luka 8:15 Luke 8:15

Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.

Luka 8:16 Luke 8:16

Hakuna mtu ambaye akiisha washa taa huifunika kwa chombo, au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuona nuru yake.

Luka 8:17 Luke 8:17

Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kutokea wazi.

Luka 8:18 Luke 8:18

Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.

Luka 8:19 Luke 8:19

Wakamwendea mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya mkutano.

Luka 8:20 Luke 8:20

Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe.

Luka 8:21 Luke 8:21

Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya.

Luka 8:22 Luke 8:22

Ikawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga.

Luka 8:23 Luke 8:23

Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.

Luka 8:24 Luke 8:24

Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari.

Luka 8:25 Luke 8:25

Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?

Luka 8:26 Luke 8:26

Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya.

Luka 8:27 Luke 8:27

Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini.

Luka 8:28 Luke 8:28

Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese.

Luka 8:29 Luke 8:29

Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo.

Luka 8:30 Luke 8:30

Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia.

Luka 8:31 Luke 8:31

Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni.

Luka 8:32 Luke 8:32

Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa.

Luka 8:33 Luke 8:33

Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi lilitelemka gengeni kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji.

Luka 8:34 Luke 8:34

Wachungaji walipoona lililotokea walikimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani.

Luka 8:35 Luke 8:35

Watu wakatoka kwenda kuliona lililotokea, wakamwendea Yesu, wakamwona mtu yule aliyetokwa na pepo ameketi miguuni pa Yesu, amevaa nguo, ana akili zake; wakaogopa.

Luka 8:36 Luke 8:36

Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza jinsi alivyoponywa yule aliyepagawa na pepo.

Luka 8:37 Luke 8:37

Na jamii ya watu wa nchi ya Wagerasi iliyo kando kando walimwomba aondoke kwao, kwa kuwa walishikwa na hofu nyingi; basi akapanda chomboni, akarudi.

Luka 8:38 Luke 8:38

Na mtu yule aliyetokwa na pepo alimwomba ruhusa afuatane naye; lakini yeye alimwaga akisema,

Luka 8:39 Luke 8:39

Rudi nyumbani kwako, ukahubiri yalivyo makuu Mungu aliyokutendea. Akaenda zake, akihubiri katika mji wote, yalivyo makuu mambo aliyotendewa na Yesu.

Luka 8:40 Luke 8:40

Basi Yesu aliporudi mkutano ulimkaribisha kwa furaha, maana walikuwa wakimngojea wote.

Luka 8:41 Luke 8:41

Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake;

Luka 8:42 Luke 8:42

kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.

Luka 8:43 Luke 8:43

Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,

Luka 8:44 Luke 8:44

alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.

Luka 8:45 Luke 8:45

Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga.

Luka 8:46 Luke 8:46

Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka.

Luka 8:47 Luke 8:47

Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.

Luka 8:48 Luke 8:48

Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani.

Luka 8:49 Luke 8:49

Alipokuwa akinena hayo, alikuja mtu kutoka nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha kufa; usimsumbue mwalimu.

Luka 8:50 Luke 8:50

Lakini Yesu aliposikia hayo, alimjibu, Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa.

Luka 8:51 Luke 8:51

Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye.

Luka 8:52 Luke 8:52

Na watu wote walikuwa wakilia na kumwombolezea; akasema, Msilie, hakufa huyu, bali amelala usingizi tu.

Luka 8:53 Luke 8:53

Wakamcheka sana, maana walijua ya kuwa amekwisha kufa.

Luka 8:54 Luke 8:54

Akamshika mkono, akapaza sauti, akisema Kijana, inuka.

Luka 8:55 Luke 8:55

Roho yake ikamrejea, naye mara hiyo akasimama. Akaamuru apewe chakula.

Luka 8:56 Luke 8:56

Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini akawakataza wasimwambie mtu lililotukia.