Luka Mlango 2 Luke

Luka 2:1 Luke 2:1

Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.

Luka 2:2 Luke 2:2

Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu.

Luka 2:3 Luke 2:3

Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao.

Luka 2:4 Luke 2:4

Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

Luka 2:5 Luke 2:5

ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba.

Luka 2:6 Luke 2:6

Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia,

Luka 2:7 Luke 2:7

akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.

Luka 2:8 Luke 2:8

Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.

Luka 2:9 Luke 2:9

Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.

Luka 2:10 Luke 2:10

Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;

Luka 2:11 Luke 2:11

maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.

Luka 2:12 Luke 2:12

Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe.

Luka 2:13 Luke 2:13

Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,

Luka 2:14 Luke 2:14

Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.

Luka 2:15 Luke 2:15

Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.

Luka 2:16 Luke 2:16

Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.

Luka 2:17 Luke 2:17

Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto.

Luka 2:18 Luke 2:18

Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji.

Luka 2:19 Luke 2:19

Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake.

Luka 2:20 Luke 2:20

Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.

Luka 2:21 Luke 2:21

Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.

Luka 2:22 Luke 2:22

Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana,

Luka 2:23 Luke 2:23

(kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto mwanamume aliye kifungua mimba ya mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana),

Luka 2:24 Luke 2:24

wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili.

Luka 2:25 Luke 2:25

Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.

Luka 2:26 Luke 2:26

Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

Luka 2:27 Luke 2:27

Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,

Luka 2:28 Luke 2:28

yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

Luka 2:29 Luke 2:29

Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;

Luka 2:30 Luke 2:30

Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,

Luka 2:31 Luke 2:31

Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

Luka 2:32 Luke 2:32

Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.

Luka 2:33 Luke 2:33

Na babaye na mamaye walikuwa wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake.

Luka 2:34 Luke 2:34

Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.

Luka 2:35 Luke 2:35

Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi.

Luka 2:36 Luke 2:36

Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.

Luka 2:37 Luke 2:37

Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.

Luka 2:38 Luke 2:38

Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.

Luka 2:39 Luke 2:39

Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti.

Luka 2:40 Luke 2:40

Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

Luka 2:41 Luke 2:41

Basi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka.

Luka 2:42 Luke 2:42

Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu;

Luka 2:43 Luke 2:43

na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari.

Luka 2:44 Luke 2:44

Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao;

Luka 2:45 Luke 2:45

na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta.

Luka 2:46 Luke 2:46

Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.

Luka 2:47 Luke 2:47

Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.

Luka 2:48 Luke 2:48

Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.

Luka 2:49 Luke 2:49

Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?

Luka 2:50 Luke 2:50

Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia.

Luka 2:51 Luke 2:51

Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.

Luka 2:52 Luke 2:52

Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.