Luka Mlango 12 Luke

Luka 12:1 Luke 12:1

Wakati huo, makutano walipokutanika elfu elfu, hata wakakanyagana, alianza kuwaambia wanafunzi wake kwanza, Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni unafiki.

Luka 12:2 Luke 12:2

Lakini hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana.

Luka 12:3 Luke 12:3

Basi, yo yote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari.

Luka 12:4 Luke 12:4

Nami nawaambia ninyi rafiki zangu, msiwaogope hao wauuao mwili, kisha baada ya hayo hawana wawezalo kutenda zaidi.

Luka 12:5 Luke 12:5

Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.

Luka 12:6 Luke 12:6

Je! Mashomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu.

Luka 12:7 Luke 12:7

Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi, bora ninyi kuliko mashomoro wengi.

Luka 12:8 Luke 12:8

Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu;

Luka 12:9 Luke 12:9

na mwenye kunikana mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu.

Luka 12:10 Luke 12:10

Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali aliyemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.

Luka 12:11 Luke 12:11

Na watakapowapeleka ninyi mbele ya masinagogi na maliwali na wenye mamlaka, msifadhaike kwa kuwaza maneno yenu jinsi mtakavyojibu au kusema;

Luka 12:12 Luke 12:12

kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.

Luka 12:13 Luke 12:13

Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu.

Luka 12:14 Luke 12:14

Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu?

Luka 12:15 Luke 12:15

Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.

Luka 12:16 Luke 12:16

Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;

Luka 12:17 Luke 12:17

akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.

Luka 12:18 Luke 12:18

Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.

Luka 12:19 Luke 12:19

Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.

Luka 12:20 Luke 12:20

Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?

Luka 12:21 Luke 12:21

Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.

Luka 12:22 Luke 12:22

Akawaambia wanafunzi wake, Kwa sababu hiyo nawaambia, Msisumbukie maisha yenu, mtakula nini; wala miili yenu, mtavaa nini.

Luka 12:23 Luke 12:23

Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.

Luka 12:24 Luke 12:24

Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, na Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!

Luka 12:25 Luke 12:25

Na yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

Luka 12:26 Luke 12:26

Basi, ikiwa hamwezi hata neno lililo dogo, kwa nini kujisumbua kwa ajili ya yale mengine?

Luka 12:27 Luke 12:27

Yatafakarini maua jinsi yameavyo; hayatendi kazi wala hayasokoti; nami nawaambia ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

Luka 12:28 Luke 12:28

Basi, ikiwa Mungu huvika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatawatendea ninyi zaidi, enyi wa imani haba?

Luka 12:29 Luke 12:29

Ninyi msitafute mtakavyokula wala mtakavyokunywa; wala msifanye wasiwasi,

Luka 12:30 Luke 12:30

kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo.

Luka 12:31 Luke 12:31

Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa.

Luka 12:32 Luke 12:32

Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.

Luka 12:33 Luke 12:33

Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu.

Luka 12:34 Luke 12:34

Kwa kuwa hazina yenu ilipo, ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu.

Luka 12:35 Luke 12:35

Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka;

Luka 12:36 Luke 12:36

nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.

Luka 12:37 Luke 12:37

Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.

Luka 12:38 Luke 12:38

Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.

Luka 12:39 Luke 12:39

Lakini fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa.

Luka 12:40 Luke 12:40

Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.

Luka 12:41 Luke 12:41

Petro akamwambia, Bwana, mithali hiyo umetuambia sisi tu, au watu wote pia?

Luka 12:42 Luke 12:42

Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?

Luka 12:43 Luke 12:43

Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo.

Luka 12:44 Luke 12:44

Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote.

Luka 12:45 Luke 12:45

Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;

Luka 12:46 Luke 12:46

bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini.

Luka 12:47 Luke 12:47

Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.

Luka 12:48 Luke 12:48

Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.

Luka 12:49 Luke 12:49

Nimekuja kutupa moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi?

Luka 12:50 Luke 12:50

Lakini nina ubatizo unipasao kubatiziwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe!

Luka 12:51 Luke 12:51

Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano.

Luka 12:52 Luke 12:52

Kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu.

Luka 12:53 Luke 12:53

Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu.

Luka 12:54 Luke 12:54

Akawaambia makutano pia, Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo.

Luka 12:55 Luke 12:55

Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.

Luka 12:56 Luke 12:56

Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya?

Luka 12:57 Luke 12:57

Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki?

Luka 12:58 Luke 12:58

Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani.

Luka 12:59 Luke 12:59

Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.