Luka Mlango 21 Luke

Luka 21:1 Luke 21:1

Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina.

Luka 21:2 Luke 21:2

Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili.

Luka 21:3 Luke 21:3

Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote;

Luka 21:4 Luke 21:4

maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.

Luka 21:5 Luke 21:5

Na watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu, alisema,

Luka 21:6 Luke 21:6

Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.

Luka 21:7 Luke 21:7

Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo ya karibu kutukia?

Luka 21:8 Luke 21:8

Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao.

Luka 21:9 Luke 21:9

Nanyi mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi.

Luka 21:10 Luke 21:10

Kisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme;

Luka 21:11 Luke 21:11

kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.

Luka 21:12 Luke 21:12

Lakini, kabla hayo yote hayajatokea, watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi, na kuwaua magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu.

Luka 21:13 Luke 21:13

Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu.

Luka 21:14 Luke 21:14

Basi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu;

Luka 21:15 Luke 21:15

kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.

Luka 21:16 Luke 21:16

Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu.

Luka 21:17 Luke 21:17

Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.

Luka 21:18 Luke 21:18

Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu.

Luka 21:19 Luke 21:19

Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.

Luka 21:20 Luke 21:20

Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia.

Luka 21:21 Luke 21:21

Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.

Luka 21:22 Luke 21:22

Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.

Luka 21:23 Luke 21:23

Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.

Luka 21:24 Luke 21:24

Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.

Luka 21:25 Luke 21:25

Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake;

Luka 21:26 Luke 21:26

watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.

Luka 21:27 Luke 21:27

Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

Luka 21:28 Luke 21:28

Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.

Luka 21:29 Luke 21:29

Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote.

Luka 21:30 Luke 21:30

Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.

Luka 21:31 Luke 21:31

Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.

Luka 21:32 Luke 21:32

Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie.

Luka 21:33 Luke 21:33

Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Luka 21:34 Luke 21:34

Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;

Luka 21:35 Luke 21:35

kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.

Luka 21:36 Luke 21:36

Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.

Luka 21:37 Luke 21:37

Basi, kila mchana alikuwa akifundisha hekaluni, na usiku huenda kulala katika mlima uitwao wa Mizeituni.

Luka 21:38 Luke 21:38

Na watu wote walikuwa wakiamka mapema waende hekaluni ili kumsikiliza.